KATEKISIMU NDOGO YA KANISA KATOLIKI

 

KATEKISIMU NDOGO KATOKILIKI


SEHEMU YA KWANZA :IMANI

1.0:NASADIKI

1. Yatupasa kusadiki nini?

 Yatupasa kusadiki uwepo wa Mungu Mwenyezi aliye hai na yote yaliyofunuliwa na Mungu. (KKK. n. 150)


1.1:KWA MUNGU BABA MWENYEZI

5. Mungu ni nani?

 Mungu ni muumba wa mbingu na dunia, muumba wa watu na wa vitu vyote na ni Baba yetu Mwema.

8. Mungu yupoje?

 Mungu ni Roho kamili kabisa. Hana mwili

20. Kuna miungu wangapi?

 Yuko Mungu mmoja tu Yuko Mungu mmoja tu.




1.2:MUUMBA WA MBINGU NA DUNIA.

25. Mungu amewaumba nani mbinguni?

 Mbinguni Mungu amewaumba malaika.

32. Mungu alisema nini alipomwumba mtu?

 Mungu alipomuumba mtu alisema: “Tumfanye mtu kwa mfano na sura yetu”


1.3:YESU KRISTU MWANAE WA PEKEE BWANA WETU ALIYETUNGWA KWA ROHO MTAKATIFU AKAZALIWA NA BIKIRA MARIA

47. Yesu Kristu ni nani?

 Yesu Kristu ni Mwana wa Mungu, nafsi a pili ya Utatu Mtakatifu, aliyejifanya mtu kwa ajili yetu ili atukomboe na dhambi na mauti

1.4:AKATESWA KWA MAMLAKA YA PONSIO PILATO  AKATESWA AKAFA AKAZIKWA AKASHUKIA KUZIMU SIKU YA TATU AKAFUFUKA KATIKA WAFU

. 65. Yesu alitukomboa kwa namna gani?

 Yesu alitukomboa kwa kuteswa, kufa na kufufuka kwake na kutuletea Roho Mtakatifu.



 AKAPAA MBINGUNI AMEKAA KUUME KWA MUNGU BABA MWENYEX

73. Yesu alipaa mbinguni lini?

 Yesu alipaa mbinguni siku ya arobaini baada ya kufufuka kwake kutoka wafu


. 75. ‘Toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu’ maana yake nini?

 Maana yake, Yesu siku ya mwisho atarudi tena duniani kuwahukumu watu wote.


78. Roho Mtakatifu ni nani?

 Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, Mungu sawa na Baba na Mwana.


81. Kanisa Katoliki ni nini?

 Kanisa Katoliki ni familia ya wakristu waliyowekwa na Yesu Kristu, yenye imani moja, chini ya Baba Mtakatifu, Askofu wa Roma.


97. Ushirika wa watakatifu ni nini?

 Ushirika wa watakatifu ni:

 i. Umoja na ushirikiano kati ya waumini wakristu duniani, watakatifu mbinguni na marehemu toharani.

 ii. Pia ni muungano wa waumini wote katika Ekaristi Takatifu.


99. Kusadiki maondoleo ya dhambi maana yake nini?

 Kusadiki maondoleo ya dhambi ni kusadiki kwamba Roho Mtakatifu, kwa huduma ya Kanisa, anaondolea dhambi zetu na adhabu zake kwa mastahili ya Yesu Kristu Mkombozi wetu.


100. Ufufuko wa miili maana yake nini?

 Ufufuko wa miili maana yake, mwisho wa dunia, kwa enzi yake Mungu, roho ya kila mtu aliyekufa itarudi mwilini mwake na watu wote watafufuka.


100. Ufufuko wa miili maana yake nini?

 Ufufuko wa miili maana yake, mwisho wa dunia, kwa enzi yake Mungu, roho ya kila mtu aliyekufa itarudi mwilini mwake na watu wote watafufuka


 104. Liturjia ni nini?

 Liturjia ni tendo, katika Roho Mtakatifu, la Kristu mwenyewe na Kanisa lake, la kumtukuza na kumwabudu Mungu Baba na hivyo kutekeleza fumbo la wokovu kwa kuwatakasa watu.


116. Neema ni nini?

 Neema ni kipaji cha kiroho tunachopewa na Mungu ili tupate kufika mbinguni.


122. Tunapata neema ya Mungu namna gani?

 Tunapata neema ya Mungu kwa imani na kwa njia ya sakramenti na sala


132. Ubatizo ni nini?

 Ubatizo (ni sakramenti inayotuwezesha kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho Mtakatifu), ni mlango (kiingilio) kwa sakramenti nyingine zote, na ni ufunguo wa uzima wa milele.


141. Kipaimara ni nini?

 Kipaimara ni sakramenti inayotuletea Roho Mtakatifu na mapaji yake ili kutufanya Wakristu imara na askari hodari wa Yesu Kristu hata tuweze kushuhudia imani yetu kwa maneno na matendo.


150. Ekaristi Takatifu ni nini?

 Ekaristi Takatifu ni sakramenti ya mwili na damu ya Yesu Kristu, Mungu- Mtu katika maumbo ya mkata na divai.


167. Kitubio na Upatanisho ni nini?

 Kitubio au Upatanisho ni sakramenti ya kuondolea dhambi tulizotenda baada ya ubatizo.


185. Mpako Mtakatifu wa wagonjwa ni nini?

 Mpako Mtakatifu wa wagonjwa ni sakramenti inayotolewa kwa wanaoelemewa na ugonjwa na uzee ili wapate neema ya pekee na faraja rohoni na mwilini, na hata waponywe ikiwa ni vema kwa wokovu wao.



191.Daraja Takatifu au Upadre ni nini?


 Daraja Takatifu au Upadre ni sakramenti inayompa mwanaume Mkatoliki uwezo mtakatifu ili:

 i. Atolee sadaka ya Misa Takatifu.

 ii. Awashirikishe watu sakramenti.

 iii. Awahubirie na kuwafundisha watu rasmi.

 iv. Awaongoze watu na kutoa baraka.


198. Ndoa ni nini?

 Ndoa ni mapatano ya mume mmoja na mke mmoja.


206. Kisakramenti ni nini?

 Kisakramenti ni:

 i. Baraka ya Kanisa juu ya watu na vitu.

 ii. Vitu vyenyewe vilivyobarikiwa, mfano: medali, rozari, maji ya baraka, majivu, matawi, misalaba, n.k.


209. Kusali maana yake nini?

 Kusali ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea naye ili kumwabudu, kumshukuru na kumwomba kwa ajili yetu na wengine.


219. Amri kubwa kuliko zote ni ipi?

 Amri kubwa kuliko zote ni amri ya mapendo kwa Mungu na jirani:

 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote na kwa nguvu  zako zote,Na ya pili ndiyo hii : Mpende jirani yako kama nafsi yako(Mk. 12:30-31)


222. Mungu alitangaza amri zake kwa maneno gani?

 Mungu alitangaza Amri zake kwa maneno haya:

 Ndimi Bwana Mungu wako :

 1.Usiabudu miungu wengine

 ii.Usilitaje bure jina la Mungu wako

 iii.Shika kitakatifu siku ya Mungu

 iv.Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani

 v.Usiue

 vi.Usizini

 vii.Usiibe

 viii.Usiseme uongo

 ix.Usitamani mwanamke asiwe mke wako

 x.Usitamani mali ya mtu mwengine


224. Kwa amri ya kwanza Mungu anatuamuru nini?

 kwa amri ya kwanza Mungu ametuamuru tu msadiki, tumtumaini,tumpende na tumwabudu Yeye peke yake aliye Bwana wa mbingu na dunia

231. Kwa amri ya tatu Mungu ameamuru nini?

 Kwa amri ya tatu Mungu ameamuru kushika kitakatifu siku ya Dominika na sikukuu za amri kwa:

 i.Kushiriki sadaja ya Misa Takatifu na mikutano ya wakristu siku za Dominika.

 ii.Kutenda mema: matendo ya huruma

 iii.Kuacha kazi ngumu (Mwa 2:1-3,Mk 2:23-28)


 234. Kwa amri ya nne Mungu ametuamuru nini?

 Kwa amri ya nne Mungu ametuamuru kuwaheshimu wazazi na wakubwa wengine , tuwapende, tuwatii katika mambo yote mema na tuwaombee(Kut 20:12,Kol 3:20)


243. Kwa amri ya Tano Mungu ametuamuru nini?

 Kwa amri ya tano Mungu ametuamuru tutunze uhai wetu na wakila binadamu wa mwili na wa roho, kwa sababu vyote ni mali ya Mungu(Mdo 17:25,28,Rum 14:7-8; KKK m 2318)




247. Kwa amri ya sita na ya tisa Mungu ametuamuru nini?

 Kwa amri ya sita na ya tisa Mungu ametuamuru kuwa waaminifu katika ndoa, kulinda usafi wa moyo(mwa. 39:7-12, Mt 5:27,Law 18 na 30)


251. Kwa amri ya saba Mungu ametuamuru nini?

 Kwa amri ya saba Mungu ametuamuru tujipatie mali kwa njia ya halali na tujali mali za wenzetu.


256. Kwa amri ya nane Mungu anatuamuru nini?

 Kwa amri ya nane Mungu anatuamuru tuseme ukweli na tulinde heshima ya wengine(Mt. 5:37, Yak 5:12)


261. Amri za Kanisa ni zipi?

 Amri za Kanisa ni sita:

 i.Shiriki Misa Takatifu Siku ya Bwana na Sikukuu zilizoamriwa.

 ii.Shiriki liturjia Jumatano ya Majivu iliyo siku ya kufunga chakula na Ijumaa Kuu iliyosiku ya kuacha kula nyama.

 iii.Ungama dhambi zako kila unapohitaji, walau mara moja kwa mwaka.

 iv.Pokea Ekaristi Takatifu mara nyingi hasa kipindi cha Pasaka. v.Shika sheria katoliki za ndoa,wala usimzuie mwana wako kufuata wito wake(ndoa,ukatekista,utawa,upandre)

 vi.Saidia kanisa katoliki kwa zaka,sadaka na kwahuduma.


269. Fadhila ni nini?

 Fadhila ni mazoea imara ya mtu kutenda mema( 1 Tim 4:6-8; KKK n. 1833)


280. Dhamiri ni nini?

 Dhamiri ni sauti ya Mungu rohoni mwetu inayotuongoza kutenda mema na kutuonya kuacha mabaya .


283. Dhambi ni nini?

 Dhambi ni kuvunja kwa kusudu amri za Mungu na za Kanisa, kwa mawazo,kwa maneno, kwa matendo na kwa kutokutimiza wajibu.


291. Asili ya Vishawishi ni nini?

 Asili ya Vishawishi ni:

 i.Maelekeo yetu mabaya .

 ii. Watu wabaya

 iii.Shetani (Mwa 3:1-6,39:7-12, Rum 7:15, 1Pet 5:8-9)


4:SEHEMU YA NNE :SALA MUHIMU.

Ishara ya Msalaba

 Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu .Amina.


Sala ya Imani

 Mungu wangu nasadiki maneno yote linayofundisha Kanisa Katoliki. Maana wewe unayesema kweli tu, umetufumbulia hayo.Unizidishie imani.Amina


Sala Kumwomba Roho Mtakatifu.

 Uje Roho Mtakatifu,unisaidie niyatambue makosa yangu niyajute kwa moyo, niyaungame waziwazi, nipate kuyaacha kweli.Amina


Imani

 Ee Yesu Kristu,Mwokozi wangu,katika karamu ya mwisho uligeuza mkatekuwa mwili wako na divai kuwa damu yakoukawapa mitume na mapadre wote uwezo wa kufanya vile vile. Nasidiki kuwa wewe umo kweli katika hostia takatifu;nitapokea mwili wako na damu yako, pamoja na roho yako na Umungu wako.Wewe mwenyewe ulisema :Huu ni mwili wangu. Ee Yesu,unizidishie imani.


Kuabudu

 Salamu,ee mwili wa Yesu, ndio mwili uliozaliwa na Bikira MAria, uliotolewa sadaka msalabani kwa ajili ya watu. Ee Yesu mpole, ee Yesu mwema, ee Yesu Mwana wa Maria! Nakuabudu uliomo moyoni mwangu, ee Mungu wangu na Bwana wangu,Mungu-Mtu na Mkombozi wangu! Pamoja na watakatifu na malaika wa mbingu nakuabudu,ee Yesu Mwana wa Mungu.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies