Rehema
kamili ni nini?
Rehema kamili ni msamaha wa kufutiwa adhabu zote za muda za dhambi.
Kuna Rehema za namna ngapi?
Rehema za namna mbili
1. Rehema kamili
2. Rehema pungufu (Rehema isiyo kamili)
Rehema hutolewa na nani?
Rehema hutolewa na Kanisa Katoliki kwa kutugawia
mastahili ya Yesu Kristo, Bikira Maria na Ya Watakatifu
Rehema ni nini?
Rehema ni msamaha au ondoleo la adhabu ya dhambi
tulizostahili sababu ya dhambi zilizokwisha ondolewa
Rehema isiyo kamili (pungufu) ni nini?
Rehema isiyo kamili (pungufu) ni msamaha wa
kupunguziwa adhabu ya dhambi
Adhabu za dhambi huondolewa kwa namna gani?
Jinsi ya kupata rehema
Adhabu za dhambi huondolewa kwa;
1. Kufanya malipizi au majuto kamili
2. Kuvumilia taabu na mateso katika maisha
3. Kuvishinda vishawishi na majaribu
4. Kusali sala mbalimbali
5. Kuomba Misa kwa ajili hiyo.
6. Kusoma neno la Mungu na kulitafakari na kulinganisha
na maisha yetu ya kila siku
7. Utakaso wa Toharani kama adhabu hizi hazikuondolewa
duniani
Kipimo cha Rehema ni nini?
Kipimo cha Rehema hutegemea uzito wa majuto na mapendo
mtu aliyonayo kwa Mungu Muumba wake.Rej (1Kor 9:11)
Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa nini?
Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa;
1. Kujua na kufuata utaratibu unaotolewa na Kanisa
Katoliki wa kupata Rehema
2. Awe katika hali ya neema ya Utakaso
3. Kufanya matendo yote yanayotakiwa kwa kupata rehema
hiyo, kwa mfano;
a). Hija au Kuhiji katika mwaka wa Jubilei katika
Kanisa lililo teuliwa na Askofu
b). Kufanya mafungo - Kama vyama vya kitume
c). Kuzuru makaburi (Kutembelea) yaliyobarikiwa
d). Katika hatari ya kufa padri hutoa rehema pamoja na
Sakramenti ya wagonjwa
e). Kusali kwa nia za Baba Mtakatifu
No comments
Post a Comment