MALAIKA NI NANI NA AINA ZA MALAIKA

MALAIKA NI NANI? 


Malaika ni viumbe walio na nguvu na uwezo mkubwa kuliko wanadamu. (2 Petro 2:​11) Wanaishi mbinguni, au katika makao ya kiroho, makao ambayo yako nje ya ulimwengu halisi. (1 Wafalme 8:​27; Yohana 6:​38) Hivyo, wanatajwa kuwa roho.​—1 Wafalme 22:21; Zaburi 18:10.

 Je kuna aina ngapi za malaika?

aji i? Na wa aina ngapi?JIBU: Ulimwengu wa malaika ni mkubwa/Mpana sana kama vile ulivyo ulimwengu wa wanadamu, Kama vile Mungu alivyotoa vipawa tofauti tofauti kwa wanadamu, vivyo hivyo alitoa vipawa tofauti tofauti kwa malaika zake,..wapo malaika wa maji,(hawa wanashughulika na mambo yote yanayohusiana na maji,mfano kuleta gharika kama wakati wa Nuhu,kutenganisha bahari kama wakati wa Musa,kusababisha au kuzuia mvua kama wakati wa Eliya , kutokeza maji mwambani kama wakati wa Wana wa Israeli jangwani, kutokeza chemichemi, kugeuza maji kuwa kitu chochote kama damu n.k.)..Na watakuja kufanya hizo kazi tena katika siku ile kuu ya Bwana baada ya kanisa kunyakuliwa..Wapo pia malaika wa moto (utawaona katika..

Ufunuo 14: 18 “Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana”

 Wapo pia Malaika wa vita, mfano Mikaeli na wenzake,kazi yao ni kudhibiti nguvu za yule adui kwa watakatifu wa Mungu.

Mikaeli (Mikhā'ēl)  maana yake “Ni nani aliye sawa na Mungu? Huyu ni Malaika mkuu aliyepambana fika na Ibilisi, Shetani na kushinda, kiasi kwamba, yule nyoka mkubwa, aitwaye Shetani, Ibilisi audanganyaye ulimwengu wote, akatupwa hata katika nchi kama tunavyosoma kwenye Maandiko Matakatifu. Rej. Uf. 12:7. Malaika mkuu Rafaeli ni mlinzi wa watu wa Mungu kwa sababu yeye ni Jemedari mkuu. Rej. Dan. 12: 1.

wapo malaika wajumbe kama Gabrieli na wenzake (Danieli 9:21) ambao kazi zao ni kuwasilisha ujumbe fulani kutoka kwa Bwana kwa watakatifu, 

Gabrieli  (Gaḇrīʾēl (גַבְרִיאֵל)) maana yake ni nguvu ya Mungu. Huyu ni kati ya Malaika wakuu saba wanaokaa siku zote mbele ya Mwenyezi Mungu kama alivyosema Malaika Gabrieli alipokuwa anajibizana na Zakaria kwa kumkumbusha kwamba, yeye alikuwa ni Gabrieli anayesimama mbele ya Mungu na ametumwa kumpasha Habari Njema ya kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji. Malaika mkuu Gabrieli ndiye aliyetumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti kwa Bikira Maria, ili kumpasha Habari Njema kwamba, atakuwa ni Mama wa Mungu. Kwa maneno machache, Malaika wakuu ndio wanaowafunulia watu siri za Mwenyezi Mungu. Rej. Lk. 1-19; Lk. 1:26-28.


Rafaeli ( רָפָאֵל, Rāfāʾēl” ) maana yake ni dawa ya Mungu inayoponya. Rafaeli ni kati ya Malaika watakatifu saba wanaopeleka sala za watakatifu, na kuingia mbele za utukufu wake aliye Mtakatifu. Mwenyezi Mungu ndiye anayepaswa kupewa heshima, utukufu na sifa. Rej. Tob. 12:15 na Ufu. 8:2. Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican wanasema katika liturujia ya hapa duniani, waamini wanashiriki, wakionja liturujia ya mbinguni, iadhimishwayo katika Mji Mtakatifu Yerusalemu, wanaouelekea kama wasafari, ambako Kristo Yesu ameketi mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu kama mhudumu wa patakatifu na wa ile hema ya kweli. Waamini wanaungana na wapiganaji wa jeshi la mbinguni kumwimbia Mwenyezi Mungu wimbo wa utukufu. Wakiwakumbuka kwa heshima watakatifu, wanatumaini kupata ushirika nao, wanangojea kwa shauku Mkombozi, Kristo Yesu, mpaka atakapojidhihirisha, Yeye ambaye ni uzima wao, ndipo nao watakapodhihirishwa pamoja naye katika utukufu. Rej. SC. 8.
wapo pia wa sifa (makerubi na maserafi) na shetani naye alikuwa kwenye hili kundi kabla ya kuasi, n.k.Hawa wapo mbele ya kiti cha Enzi cha Mungu milele,

Isaya 6: 1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake”. 

kwahiyo wapo wengi hata wengine hatuwajui, na wala hatujawahi kuwaona, wapo wanaoshughulika na ULINZI tu,soma Zaburi 91: 11 “Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote”.

Kutoka 23:20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.”

Wapo malaika wa kila nchi, wapo wa kila mkristo mmoja mmoja, na wapo wanaosimama kwa kila huduma, n.k kila mmoja anatenda kazi kulingana na alivyopangiwa na Mungu mwenyewe…Wapo pia malaika wa Uponyaji, (Yohana 5:15). 

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies