MAPAJI SABA YA ROHO MTAKATIFU

YAFAHAMU MAPAJI SABA YA ROHO MTAKATIFU




1. Hekima
Ni kipaji cha Roho Mtakatifu cha kutusaidia tupende na kufurahia mambo ya Mungu.

2. Akili
Ni mwanga wa Roho Mtakatifu wa kutusaidia tumjue zaidi Mungu na ukamilifu wake pamoja na kuelewa ufunuo wake.

3. Shauri
Ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotuelekeza kuchagua siku zote mambo yenye kufaa zaidi kwa sifa ya Mungu na kwa wokovu wetu.

4. Nguvu
Ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotutia moyo wa kushika sana amri za Mungu na mambo ya utumishi wake tusiogope watu wala matukano wala mateso wala kufa.

5. Elimu
Ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotutia maarifa ya mambo ya ulimwengu huu, kwa kutambua mapungufu yake pamoja na mitego, werevu na udanganyifu wa shetani akitujaribu mwenyewe au kwa kupitia vitu kama watu.

6. Ibada
Ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotufanya tumpende Mungu kama Baba yetu mwema na watu wote kama ndugu; kwa msingi huo kutimiza utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na heshima.

7. Uchaji wa Mungu

Ni kipaji cha Roho Mtakatifu kinachotutia hofu ya kumchukiza Mungu kwa dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumtia baba yake uchungu.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies