MIZIZI SABA YA DHAMBI AU VILEMA VYA DHAMBI

Mizizi ya dhambi, au vilema vikuu au vichwa vya dhambi ni orodha ya maovu ambayo tangu zamani za mababu wa Kanisa katika maadili ya Ukristo yanahesabiwa kuelekeza binadamu kutenda dhambi nyingine, hata kubwa zaidi.Kwa kawaida inatajwa kuwa saba, zote zikitokana na umimi usiozingatia ukweli.

UBINAFSI

ni tabia ya kujijali kupita kiasi, bila kutia maanani vya kutosha watu wengine na jamii kwa jumla.Ni kinyume cha ukarimu na unamfanya mtu azingatie mnokinachompendeza au kinachomfaidisha yeye, badala ya kulenga pia kinachowafaa wengine.
Zipo aina saba za mizizi ya dhambi:

1.Majivuno
Ni tabia ya mtu kujipongeza mno kutokana na sifa alizonazo.
Yanatokana na kiburi na kufikia hatua ya majigambo ya uongo ambayo ni chukizo kwa wengine.
Katika maadili ni kimojawapo kati ya vilema vikuu (au vichwa vya dhambi) vinavyozaa dhambi nyingine nyingi.

2.Ubahili
Ni hamu isiyoratibiwa ya kujipatia mali kuliko mtu anavyohitaji, hata kuwakosesha wengine.Ni chanzo cha maovu mengi katika maisha ya jamii, kama vile unyonyaji, wizi, vita n.k.

3.Hasira
Ni ono linalowapata binadamu na wanyama mbele ya kipingamizi. Katika hali hiyo mtu hughadhibika, hata kuchukia kwa kupatwa na kitu ambacho yeye mwenyewe hapendi.Mtu mwenye hasira ya mara kwa mara, hushauriwa ajaribu kuepuka mambo au vitu vinavyomuudhi, kwa mfano, anaweza kuondoka mahali penye maudhi, na kama ni kubishana aweze kunyamaza ili kuepukana na ugomvi.
Pia inashauriwa kuwa, kama unajua mwenzio hukasirishwa na kitu fulani, bora usimchokoze, kwa sababu ni hatari kwa maisha yako maana kwa hasira yake anaweza kufanya kitu chochote kibaya.
Isiporatibiwa na mhusika inaweza ikasababisha madhara makubwa, inavyofundisha mithali ya Kiswahili, "Hasira, hasara". Hasira hupelekea mtu kuvunja sheria kwa kujichukulia hatua mkononi na mwishowe kufanya jambo la hatari.

4.Wivu

Ni hisia au kilema kinachomfanya binadamu asikitikie mambo mema waliyonayo wengine.
Kutokana nacho mtu anawatenda namna isiyopendeza na kusababisha matatizo makubwa katika maisha ya jamii.Kijicho ni hisia au kilema kinachomfanya binadamu asikitikie mambo mema waliyonayo wengine.

5.Ulafi (pamoja na ulevi)
Ni hamu isiyoratibiwa ya kula (na kunywa).Tabia hiyo ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu.Inakadiriwa kuwa siku hizi mtu 1 kati ya 3 anakula kuliko mwili wake unavyohitaji, na hivyo anasababisha maradhi mbalimbali yampate.

6.Uzinzi

Ni hamu isiyoratibiwa ya ashiki katika maisha ya binadamu.Kwa kawaida watu wanakubaliana kwamba utafutaji wa ashiki unahitaji kuwa na mipaka, hasa usilenge ndugu wa damu.

Katika maadili unaorodheshwa kati ya vilema vikuu vilivyo mizizi ya dhambi nyingine, Biblia inavyoonyesha wazi katika habari ya mfalme Daudi kuzini na mke wa askari wake Uria Mhiti (2SamUzinifu ni hamu isiyoratibiwa ya ashiki katika maisha ya binadamu.

Kwa kawaida watu wanakubaliana kwamba utafutaji wa ashiki unahitaji kuwa na mipaka, hasa usilenge ndugu wa damu.
Katika maadili unaorodheshwa kati ya vilema vikuu vilivyo mizizi ya dhambi nyingine, Biblia inavyoonyesha wazi katika habari ya mfalme Daudi kuzini na mke wa askari wake Uria Mhiti (2Sam)

7.Uvivu
Ni kukosa uwajibikaji na umakinifu katika kutenda.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies