NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

 NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

SALA KABLA YA KUINGIA KATIKA MFUNGO/NOVENA



NOVENA SIKU YA KWANZA
20/04/2020
SIKU YA KWANZA
🛐🛐🛐🛐
SALA KABLA YA KUINGIA MFUNGO/NOVENA
Ee Mungu Baba mwenyezi uliyetufanya wanadamu kwa neema yako na ukataka tukurudie wewe kwa mioyo iliyotakata. Wewe ulisema sifurahi kifo cha mtu mwovu bali auache mwenendo wake mbaya apate kuishi. Ee Bwana wewe wajua kuwa hali yetu ya kibinadamu ni dhaifu, ndio maana ulituambia tubuni na kuiamini Injili. Mara kwa mara tunaahidi kuenenda katika uzima mpya kwa kukufuata wewe, lakini tena na tena tunajikuta tumeanguka dhambini kwa ajili ya ulegevu wa mwili. Badala ya kuichukua misalaba yetu na kumfuata Kristo, tunarudi nyuma na kuanguka tena dhambini. Uturehemu ee Bwana kwa ajili ya dhambi tunazozitenda.
Kwa maombezi ya Mt. Rita wa Kahisha, mama aliyesali sana, kufunga kwa muda mrefu, na kuutesa mwili wake, unisaidie niweze kufunga chakula na starehe, niache kutenda dhambi na furaha zilizozoea. Nijibidishe kutenda matendo ya huruma na kusali zaidi. Unipe ujasiri wa kuvumilia mateso na maumivu ya mwili yakayotokana na mfungo huu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.
🛐🛐🛐🛐

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


NOVENA YA MT RITA SIKU YA KWANZA
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
SAA 1.00 ASUBUHI
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ee Mtakatifu Rita mfanya miujiza, uniangalie kwa macho yako yenye huruma, mimi ninayeteseka na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka damu umezungukwa na miiba. Yaone macho yangu, Ee Mtakatifu Rita, kuwa hayatoki machozi tena, kwani machozi mengi yamenitoka!
Nimechoka na kukata tamaa. Nimechoka pia kusali. Je, nikate tamaa katika misukosuko hii ya maisha yangu? Uje! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa? Basi dhihirisha ukuu wa jina hilo, kwa kunijalia toka kwa Mungu yote ninayokuomba
(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Kila mtu anasifia utakatifu wako. Kila mtu anasimulia maajabu na miujiza Mungu anayotenda kwa njia yako. Je, mimi tu nitakataliwa na kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uniombee kwa Bwana Yesu ili anionee huruma na kunisaidia katika masumbuko na mahangaiko yangu. Kwa maombezi yako, Ee Mtakatifu Rita, niweze kupokea kile ambacho moyo wangu unatamani sana
Baba Yetu ......(3),
Salamu Maria...... (3) na
Atukuzwe Baba...... (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.…..
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.…..
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.…..
Kiongozi: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE: Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima
🛐🛐🛐🛐

*LITANIA KWA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA*
------------------------------
Bwana Utuhurumie,
Kristo Utuhurumie,
Bwana Utuhurumie,
------------------------------
*Kiitikio *"Utuhurumie"*
Baba wa Mbinguni, Mungu,
Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,
------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Maria Imakulata Mama wa Mungu
Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka
Maria, Malkia wa Watakatifu wote
Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni:
Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu:
Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu:
Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako:
Mt Rita, mpenda upweke:
Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo:
Mt Rita, kielelezo cha upole wote:
Mt Rita, kielelezo cha mke mwema:
Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu:
Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli:
Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia:
Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa:
Mt Rita, kioo cha utii;
Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa;
Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka;
Mt Rita, shahidi katika kufanya toba
Mt Rita, mjane mtakatifu;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu;
Mt Rita, aliyeingizwa utawani kimuujiza;
Mt Rita, harufu nzuri ya manemane;
Mt Rita, bustani ya kila fadhila;
Mt Rita, mpendezwa na Yesu Msulubiwa;
Mt Rita, uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso;
Mt Rita, binti mpendevu wa Bikira Maria;
Mt Rita, mwenye kiu ya upendo wa Kimungu;
Mt Rita, uliyevikwa utukufu;
Mt Rita, lulu ya mbinguni;
Mt Rita, utukufu wa shirika la Mt Augustino;
Mt Rita, tunu ya thamani ya Umbria;
Mt Rita, mwenye nguvu za utakatifu;
Mt Rita, msamaha wa wanaopata mahangaiko;
Mt Rita, mfariji wa wanaoteseka;
Mt Rita, nanga ya wokovu;
Mt Rita, mwombezi wa wagonjwa;
Mt Rita, mwombezi wa mambo yaliyoshindikana;
Mt Rita, kimbilio la walio hatarini;
Mt Rita, msaada wenye nguvu kwa wote;
Mt Rita, mastaajabio ya ulimwengu;
Mt Rita, uliyepokewa mbinguni kwa furaha;
-----------------------------------
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusamehe Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusikilize Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia *"Utuhurumie"*
----------------------------------
*K:* Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
*W:* Kwa mhuli wa upendo na mateso
*TUOMBE*:
Ee Mungu , ambaye katika wema wako wa daima, umependa kusikiliza maombezi ya mtumishi wako Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale ambayo yameshindikana kwa nguvu za kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka, uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
------------------------------------

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies