ROHO MTAKATIFU NI NANI

MAANA YA ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE
Biblia inatwambia kwamba kuna Mungu mmoja mwenye nafsi tatu; Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Na kila moja ya nafsi ina huduma yake. Mungu Baba aliumba ulimwengu na anaendelea kuutunza. Na Mungu Mwana alizaliwa katika mwili wa binadamu na kuaokoa ulimwengu kutoka katika dhambi. Roho Mtakatifu anaamsha na kujenga imani ndani ya mwanadamu. Kwa hiyo lazima tuulize “Roho Mtakatifu ni nani?" Kwa sababu Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu na wala sio nguvu inayojitegemea.

Roho Mtakatifu anafanya kazi kati ya mtu akiamsha na kuimarisha imani katika Yesu. Anafanya kazi kupitia vyombo vya Neema: neno la Mungu, Ubatizo na Meza ya Chakula cha Bwana (sacramenti) na ungamo la dhambi; hivi ni vyombo vya Neema.

Yesu alimwita Roho Mtakatifu “Roho wa Ukweli
” na Mlinzi, kama Roho wa ukweli, Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa Biblia kuandika katika mapenzi ya Mungu, na yeye anatupa kuelewa pale tunaposoma Biblia . Kama Mlinzi anatuhakikishia katika roho zetu kwamba Mungu ni wa rehema kwetu kupitia Yesu Kristo ijapokuwa tumeanguka na kustahili adhabu.

Ndani ya waamini Roho Mtakatifu anatoa uzima ambao unatokana na mapenzi ya Mungu na pia anatoa zawadi za Roho kulijenga Kanisa.


“Lakini ajapo huyo msaidizi nitakayewapelekea, kutoka kwa Baba, yaani Roho wa kweli, atokaye kwa baba yeye atanishuhudia"
(John 15:26, )

UNAWEZA KUWA NA ROHO MTAKATIFU?


Roho Mtakatifu anaweza kuishi ndani ya mwanadamu, hakika, kila muumini katika Yesu Kristo ana Roho Mtakatifu. Pasipo Roho Mtakatifu hakuna anayeweza kuamini. Mojawapo ya mambo yasiyoeleweka ya ukristo ni kwamba Mungu mwenye nguvu anatamani kuishi ndani ya moyo wa mwanadamu mdogo na mwenye dhambi.

Roho Mtakatifu anakuja kwenye moyo wa mwanadamu kupitia Neno la Mungu na kupitia sakramenti ya ubatizo na sacramenti ya Meza ya Bwana. Kwa Kutumia hivi vyombo vya Neema anaamsha imani ya kweli (uokoayo) ndani ya Yesu Kristo katika Moyo wa mwanadamu na kumfanya mtoto wa Mungu. Mtoto wa Mungu hata hivyo anaweza kukosa utii na kumhuzunisha Roho Mtakatifu na kuanguka katika kutoamini. Hii ndio maana Biblia inaonya kuhusu watu wenye mioyo migumu, na waasi na wanaojiinua, wapate kurudi tu kwa Mwokozi.


“Lakini Roho wa Mungu anakaa ndani yenu ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake”
(Warumi 8:9,)

KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU INAMAANA GANI?


Wakati wasomi wanapinga kwamba Yesu alifanyakazi kwa kupitia nguvu za shetani, Yesu aliwaonya kuhusu kumkufuru Roho Mtakatifu. Kumkufuru Roho mtakatifu ni dhamira ya kinyume ya kazi za Roho Mtakatifu. Kuna mifano mahali pengine katika Biblia pia, katika barua ya kitabu cha Waebrania anazungumzia dhambi ya dhamiri ambaye ina kupelekea katika utengano na Mungu. Kwa njia hii haizungumzia dhambi nyingine ila ni dhambi inayokufanya ukatae imani.

Maneno ya Yesu katika waraka kwa Waebrania usieleweka kama kushutumu mtu yeyote lakini kama onyo kwa wale wote ambao hawajafanya dhambi hii. Ni muhimu kukumbuka kwamba mlango wa Mungu upo wazi kwa kipindi hiki ambacho injili ya Yesu Kristo inahubiriwa. Na shida kwa mtu ambaye alifanya dhambi ya kukufuru Roho Mtakatifu kwamba Mungu atasamehe au la! Lakini haya ni kutokuwa na mapenzi kumrudia Mungu – Moyo umefanya mgumu. Kwa hiyo yeyote anayeogopa kutenda dhambi ya kurudia anaweza kuwa na hakika kwamba hajafanya hiyo dhambi kwa sababu toba ni alama ya moyo ambao bado unaskiliza wito wa Mungu.

“Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa na katika ule ujao.
(Mathayo 12:32,)

Bwana YESU alitutangazia kuja kwa ROHO MTAKATIFU, hii iko Yohana 14:26 ”Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Sasa tuangalie lengo mahususi la ujio wa Roho Mtakatifu kwetu;


1). Alikuja ili awe msaidizi wetu na kukaa nasi
. Yeye anatusaidia katika maisha yetu mambo mengi. “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye Roho wa kweli…”Yohana 14:16, 17.

2). Kutusaidia kuomba.
“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” Warumi 8:26, 27.

3). Kutuongoza na kutuambia mambo yajayo.
“Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatoa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu, kwa hiyo nalisema ya kwamba atatoa yaliyo yangu na kuwapashani habari” Yohana 16:13-15.“Kwa kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” Warumi 8:14. Neno linaonyesha wazi wanaongozwa na Roho mtakatifu ni wana wa Mungu, ambao wamekwishafanyika watoto wa Mungu kwa kumpokea Yesu. “Bli wote waliompokea waliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” Yohana1:12.

4). Kutufundisha na kutukumbusha
.“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” Yohana 14:26.

5). Kutumiminia pendo la Mungu katika mioyo yetu
.“…kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu aliyetupa sisi” Warumi 5:5.

6). Kuuhakikishia ulimwengu dhambi, haki na hukumu.
“…huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampoeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu” Yohana 16:7,8. Roho Mtakatifu anauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu wakati watumishi wa Mungu wanapohubiri na kufundisha neno la Mungu.

7 ) .Kutushuhudia kuwa watoto wa Mungu
.“Roho mwenyewe hutushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.” Warumi 8:16.Ukiishi sawasawa na neno la Mungu Roho mtakatifu anakushuhudia ndani yako ya kwamba wewe ni mtoto wa Mungu. Kama neno la Mungu linavyofundisha waliompokea Yesu walipewa haki ya kuwa watoto wa Mungu. Lakini haki hii hawakuipa bila kujitolea au kujikabidhi kwa Mungu. Walimgeukia Mungu na kuacha maovu yote kwa kutubu na kusamehewa, ndio maana walifanyika watoto wa Mungu.






No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies