SAKRAMENT ZA KANISA


JE SAKRAMENTI ZIPO KATIKA MAANDIKO?.

Kulingana na Kanisa Katoliki Sakramenti Ni ishara ya wazi ionekanayo, ya neema isiyoonekana, iliyofanywa na Yesu Kristo mwenyewe, itumike kutuletea au kutuongezea neema mioyoni mwetu.
Yaani kwa lugha nyepesi ni ishara za nje zionekanazo zilizobeba neema ya wokovu, zilizofanywa kwanza na Bwana Yesu, ambazo tukizifanya na sisi zitatuongezea neema moyoni mwetu ya kumkaribia Mungu zaidi.
“Kulingana na Kanisa Katoliki SAKRAMENTI hizi zipo saba (7), Nazo ni:
1:UBATIZO
Kwamba kila mtu anayekuja katika ukristo ni sharti aupokee ubatizo, haijalishi ni Watoto wachanga, au vijana,au watu wazima, hawana budu kuupokea ubatizo. Ni ishara ya nje ya kuingizwa katika imani ya kikristo. Hii ni sakramenti ya kwanza.[Rejea Yn3:3 na Mk16:15-16]
2:KIPAIMARA
Kipaimara ni Neno lenye maana ya “uthibitisho”. Kulingana na imani ya kikatoliki, ubatizo peke yake hautoshi, unahitaji kukamilishwa na tendo lingine la kipaimara kwa kuwekewa mikono. Hivyo Siku ambayo mtu huyo anapokea kipaimara hicho huwa anapakwa mafuta ya kunukia kwenye paji la uso wake yajulikanayo kama KRISMA, kama ishara ya kutiwa muhuri kuwa mtu huyo ni milki halali ya Bwana, kufuatana na andiko hili.[ Rejea Yohana 6:27 na Mdo 8:14-17]
3:EKARISTI TAKATIFU
Kushiriki meza ya Bwana. Kuula mwili wa Bwana na damu yake.. (1Wakorintho 11:23-25). Kama vile Bwana Yesu alivyowaagiza wanafunzi wake wafanye vile kwa ukumbusho wake.

4:KITUBIO
Inahusisha kuungama dhambi, na hii ni lazima uende mbele za Padri na kuzikiri dhambi zako mbele zake, na yeye atakuombea na dhambi zako zitaondolewa kama agizo ambalo Kristo aliwapa mitume wake..[Yohana 20:23].

5:MPAKO MTAKATIFU:
Hii ni ibada maalumu kwa ajili ya wagonjwa kama ilivyofanywa na mitume kwa agizo la Yakobo (Yakobo 5:14) ..Mathayo 10:1, Marko 6:3…Hii nayo ni moja ya sakramenti ya Bwana.
6:DARAJA TAKATIFU-UPADRE
Uteuzi wa Vyeo katika kanisa..kama vile ukasisi, ushemasi, na uaskofu.Kama vile jinsi Bwana Yesu alivyowachagua mitume wake,.Na vivyo hivyo uteuzi katika kanisa ufanyike katika kuliongoza kundi, hiyo inafuatana na kuteuliwa na kuwekewa mikono na askofu wa jimbo.[Rejea Lk 22:21-25 na 1Kor 11:24-25]

7:NDOA
Ndoa ya wakristo ni sakramenti ya Yesu na kanisa lake. Ufunuo 21;9..Kama vile Kristo alivyoona na kanisa lake, vivyo hivyo ndoa inafunua sakramenti hiyo.[Rejea Mwa 2:21-25 na Mt 19:3-9].



No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies