Sala ya saa Tisa

✝⌚✝


Sala ya saa tisa



Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. A mina



Yesu, ulikufa, lakini chanzo cha uhai kilitoka kwa ajili ya watu, na bahari ya huruma ilifunguka kwa ajili ya ulimwengu mzima. Ee chemchemi ya Uhai, huruma ya Mungu isiyo na mwisho, ikafunika ulimwengu mzima na ukajimwaga mwenyewe juu yetu.


❣✝❣



✝Ee Damu na Maji, yaliyotoka moyoni mwa Yesu kama chemchemi ya Huruma kwetu. Nakutumainia.


(Mara tatu)


🛐❣🛐



ROZALI YA HURUMA YA MUNGU (MUONGOZO MPYA)


✝Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu....


✝✝✝✝

Tumia chembe za rozari ya kawaida au Rozari ya Huruma ya Mungu 


✝✝✝✝

 *Sali Baba Yetu Mara x1*

 

Baba yetu, uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie kishawishini bali utuopoe maovuni. Amina.


✝✝✝✝

 *Sali Salamu Maria Mara (1)* 

Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.


✝✝✝✝

Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, uzima wa milele. Amina.


✝✝✝✝

 *Kila penye punje kubwa* 

Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi na Bwana wetu Yesu Kristo, kwa malipizi ya dhambi zetu, na za dunia nzima.


✝✝✝✝

 *Kila penye punje ndogo*  :

Kwa ajili ya mateso  yake makali..... Utuhurumie sisi na dunia nzima.


✝✝✝✝

 *Mwisho wa Rozari* 

 *sali mara tatu (3)sala ifuatayo* : 


Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu Usiyeweza kufa...... Utuhurumie sisi na dunia nzima.


✝✝✝✝


 Litania ya Huruma ya Mungu


⏹Bwana utuhurumie 

⏺Bwana utuhurumie

⏹Kristu utuhurumie ⏺Kristu

utuhurumie

⏹Bwana utuhurumie 

⏺Bwana utuhurumie

⏹Kristu utusikie 

⏺Kristu

utusikilize


Baba wa mbinguni Mungu –

utuhurumie


Mwana Mkombozi wa dunia

Mungu - utuhurumie


Roho Mtakatifu Mungu -

utuhurumie


Utatu Mtakatifu Mungu mmoja –

utuhurumie.


Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu

ya Muumba wetu -

 *Tunakutumainia*-(iwekiitikio)


Huruma ya Mungu iliyo kilele cha

ukamilifu wa Mwokozi wetu-


Huruma ya Mungu iliyo upendo

usiopimika wa Roho Mtakasa


Huruma ya Mungu fumbo

lisilofahamika la Utatu Mtakatifu


Huruma ya Mungu iliyo ishara ya

uwezo mkuu wa Mungu

Mwenyezi


Huruma ya Mungu

iliyofumbuliwa katika kuziumba

Roho za Malaika wa mbinguni


Huruma ya Mungu iliyotuumba

na kutuamuru tuwepo bila

kutokana na chochote


Huruma ya Mungu inayotujalia

maisha ya kutokufa


Huruma ya Mungu inayotukinga

na adhabu tunazostahili


Huruma ya Mungu inayotuinua

tutoke katika taabu, unyonge na

maumivu ya dhambi zetu


Huruma ya Mungu inayotufanya

wenye haki katika Neno

aliyejifanya Mtu


Huruma ya Mungu inayofurika

kutoka katika majeraha ya Kristu


Huruma ya Mungu inayobubujika

kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu

wa Yesu


Huruma ya Mungu iliyotupatia

Bikira Maria Mtukufu awe kwetuMama wa Huruma


Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa

katika kuanzishwa Kanisa Katoliki


Huruma ya Mungu inayopatikana katika mafumbo ya Sakramenti

Takatifu


Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio


Huruma ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho


Huruma ya Mungu

inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika

kuwatakatifuza wenye haki


Huruma ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watu

watakatifu


Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa na wote

wanaoteseka


Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungu moyoni


Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa na

mkato wa tamaa


Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watu wote


Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake


Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa


Huruma ya Mungu iliyo

burudisho na faraja yao

marehemu wa toharani


Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifu wote


Huruma ya Mungu iliyo taji la Watakatifu wote


Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka


Mwanakondoo wa Mungu

uliyetuonyesha huruma yako kuu katika kuikomboa dunia kwa

msalaba wako mtakatifu, -utusamehe ee Bwana


Mwanakondoo wa Mungu

unayejitolea kwetu kwa mapendo na huruma katika kila adhimisho

la Sadaka ya Misa Takatifu,-utusikilize ee Bwana

Mwanakondoo wa Mungu

anayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya huruma yako isiyo

na mwisho,- utuhurumie.


✝✝✝✝

 *Kiongozi* :

 ⏺Bwana utuhurumie

⏹ Bwana utuhurumie

⏹ Kristu utuhurumie,

⏺ Kristu Utuhurumie  ⏹Bwana utuhurumie.

⏺Bwana utuhurumie


 *Kiongozi* : Huruma anana za

Bwana zi juu ya kazi zake zote 


 *Wote* : Huruma za Bwana

nitaziimba milele.


 *Tuombe* :


✝✝✝✝Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo wako

hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako huku

duniani na kutuongezea huruma yako tena na tena, ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata mara moja, haidhuru tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima  kuzielekea na kuzishika amri zako, kwa

matumaini na kutimiza mapenzi yako matakatifu, ambayo ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu

Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na

kutawala nawe, na Roho

Mtakatifu, kwa pamoja

mkituonyesha huruma, daima na milele


 Amina🙏🏼.


 *Sala ya Kuomba Huruma ya Mungu* 


"Nakimbilia Huruma yako, Ee Mungu mwenye Huruma, uliye pekee mwema. Ingawa dhiki ni kubwa na makosa yangu ni mengi, naitumainia Huruma yako, kwani Wewe ni Mungu wa Huruma na tangu milele haijasikika kamwe, wala Mbingu wala Nchi hazikumbuki  kuwa uliicha roho yoyote iliyotumaini Huruma yako.

Ee Mungu wa Huruma, ni wewe tu uwezaye kunihesabia haki. Ni wewe usiyeweza kunikataa nitubupo na kuukaribia Moyo wako wenye Huruma ambao haujamkatalia mtu yeyote hata kama ana dhambi nyingi kiasi gani. Kwa kuwa Mwanao alinihakikishia:, " Mbingu na Nchi zingetoweka kwa haraka zaidi kuliko Huruma yangu kukataa kuikumbatia roho iliyo na matumaini"

Ee Yesu, Rafiki wa moyo mpweke ulioachwa, Wewe ni bandari yangu. Wewe ni Amani yangu, Wewe ni Wakovu wangu, Wewe ni utulivu wangu wakati wa mapambano na katikati ya bahari ya mashaka. Wewe ni mwali mwangavu umulikao njia ya MAISHA yangu. Wewe U kila kitu kwa roho iliyo pweke. Hata roho ikinyamaza, Wewe waijua na kuhifahamu. Unajua udhaifu wetu na unatufariji na kutuponya kama mganga mwema ukituondolea maumivu  Ewe uliye stadi wa kazi... Amina


*SALA YA KUOMBA MSAMAHA WA DHAMBI*



*Ee Mungu Baba Najitambulisha kwako nilivyo kwa undani wangu, ee Kuhani Mkuu wa milele. Nikisema, dhambi zangu nazielewa. Kwa kweli, mimi udhambi wangu nauelewa, ila basi nauelewa kijuujuu tu, sio kama unielewavyo Wewe, wala tena kama mimi mwenyewe nijulikanavyo kwako, Wewe mwenye maoni yaangazayo kupita jua, wewe uchunguliaye mapito ya wanadamu ukipenya mpaka ndani ya nyoyo zao*


*Ee Mungu, hata huu moyo wangu unayo kasoro ndani yake na wasiwasi mwingi hivyo, kwa jinsi hata mimi mwenyewe napata kuujua kwa shida tu. Lakini Wewe, Bwana, wafahamu maumbile yetu ya kibinadamu*


*na pia maumbile ya vitu vyote, mpaka undani wa hulka yao. Unauelewa kabisa moyo wangu na udhambi wake. Unisamehe basi, Mungu wangu, unisamehe tu*


 Amina.....



_*HURUMA YA MUNGU NI YA MILELE*_


*Kwa jina la Baba na La Mwana na la Roho Mtakatifu*,



✝✝✝✝

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies