SIKU YA NNE : JUMATATU NOVENA YA ROHO MTAKATIFU

 

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU 

SIKU YA NNE, JUMATATU


ROHO MTAKATIFU ANALIUNGANISHA KANAtakapokuja huyu Roho wa kweli , atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yn 16:13)

Baada ya kusema hayo, Yesu aliinua macho yake kuelekea mbinguni akasema “Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha kazi uliyonipa niifanye. Naomba ili wote wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba Wewe ulinituma (Yn 17:4,21).
Nasi twamuomba Mungu Mwenyezi alijalie kanisa lake umoja wa kweli, awaunganishe wakristu wa madhehebu yote katika zizi moja chini ya mchungaji mmoja.
Popote duniani watu wengi, makundi kwa makundi wanavutwa na neema hiyo ya kuungana na kuufikia umoja wa Kanisa. Hata ndugu zetu waliotengana nasi wanazidi kukubali mwongozo wa Roho Mtakatifu na kutaka kurudi katika nyumba ya Baba na kuwa kundi moja chini ya mchungaji mmoja. Isitoshe, hata sasa tena twaweza kuona kwamba kwa namna fulani wamejiunga nasi katika Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kumshuhudia hata kwa kumwaga damu yao.Tena katika hao ndugu zetu waliojitenga, Roho Mtakatifu analisha katika mioyo yao ile ya imani inayowaunganisha wafuasi wote wa Kristu. Tumwombe basi Mwenyezi Mungu atujalie hima huo umoja wa Kanisa lake tunaouania mno.
1. Ee Yesu Bwana wetu wewe umetuombea kwa Mungu Baba tuwe itu kimoja kama Wewe ulivyo kitu kimoja na Baba. Utujalie huo umoja, ili ulimwengu uone na kukiri kwamba ndiwe Bwana na Mkombozi wa watu wote
W. Twakuomba utusikie
2. Ee Yesu utujalie moyo wa kulishika neno lako kwa uaminifu, wala usituache kufuata njia zetu sisi wenyewe na kufarakana.
W. Twakuomba utusikie
3. Ee Yesu uliye Mchungaji wetu mwema, ondoa ndani yetu ile tabia ya utengano, tupate kuwa sote kundi moja chini yako wewe uliye mchungaji wetu mmoja.
W. Twakuomba utusikie
4. Ee Yesu, uliye Mchungaji mkuu, uwajalie wachungaji wetu wawe siku zote na upendo wa Jina lako, wasichoke kulichunga vema kundi lako hapa duniani na kuliweka pamoja lisitengane
W. Twakuombaa utusikie
5. Ewe Roho Mtakatifu, uziangaze akili za watu wote, wapende siku zote kuishi kwa amani, umoja na mapendano
W. Twakuomba utusikie
6. Ee Mungu, utufungulie …… wa muungano wako wa kweli sisi tulio ndugu katika Bwana wetu Yesu Kristu.
W. Twakuomba utusikie
7. Utujalie mapatano na amani, tudumu tumeungana katika familia zetu, katika jimbo letu na katika nchi yetu yote.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE;

Ee Mungu, utuunganishe sisi kondoo wako tuliotawanyika, tuwe chini ya Mwanao mpenzi, tupate sote kuushiriki ule utawala wako wa kweli na haki, utawala wa neema na amani, utawala wa upendo wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu W. Amina

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU …. (soma hapo juu)

Atukuzwe Baba…..x3






No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies