KUWAOMBEA

 FAHAMU KUHUSU KUWAOMBEA MAREHEMU!





Kanisa Katoliki limekuwa na desturi ya kuombea marehemu wote kila ifikapo mwezi wa 11,

Mwezi ambao huitwa (mwezi wa kuombea Marehemu)

Tendo hili limekuwepo tangu enzi za mababu, lilitumika katika kuwaombea msamaha kwa Mungu marehemu wao walio kufa bila kujiandaa!

2 Wamakabayo 12:38-45 (inafafanua)

"....... 43. Pia alichangisha fedha kutoka kutoka kwa watu wake fedha ipatayo drakma elfu mbili, akaipeleka Yerusalemu kwa ajili ya dhabihu ya kuondoa dhambi. Yuda alifanya tendo hilo jema kwa sababu aliamini juu ya ufufuo wa wafu.
44. Kama asingekuwa na imani kwamba; wafu watafufuliwa, ingekuwa ni upumbavu na kazi bure kuwaombea marehemu.
45. Lakini akiwa anatazamia tuzo nzuri waliowekewa waliokufa wakiwa waaminifu kwa Mungu, hilo lilikuwa wazo jema na takatifu. Kwa hiyo Yuda alitolea dhabihu ya upatanisho ili watu wapate kuondolewa dhambi zao.

Pamoja na kuendelea kuwaombea, kanisa liliweka siku maalumu ya kuombea marehemu mnamo #mwaka_968
Ambazo mpaka sasa tunaendelea kuazimisha.

Tangu mwanzoni, Kanisa limeheshimu kuwakumbuka marehemu na kutolea sala kwa ajili yao, na juu ya yote sadaka ya Ekaristi, ili waoshwe, waweze kupata heri ya mwanga wa Mungu.

Kanisa pia linahimiza kutolea sadaka, rehema, na kazi za toba kwa niaba ya marehemu (KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI, 1032).

SALA: Mungu mwenye nguvu na huruma, umefanya kifo kiwe mlango wakuingia uzima wa milele. Uwatazame kwa huruma ndugu zetu marehemu, wafanye wawe pamoja na Mwanao kwa mateso na kifo, ili, wakiwa wamefunikwa na damu ya Kristo, waweze kuja mbele zako wakiwa huru kutoka katika dhambi. Yesu nakuamini wewe. Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies