MASOMO YA MISA 20 JUNE 2023

 MASOMO YA MISA JUMANNE

SOMO1

2Kor 8:1-9

Ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu. Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu. Hata tukamwonya Tito kuwatimilizia neema hii kwenu kama vile yeye alivyotangulia kuianzisha. Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia. Sineni ili kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu. Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.



Wimbo wa Katikati

Zab 146:2, 5-9

Nitamsifu Bwana muda ninaoishi,

Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.

(K) Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.


Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,

Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake,

Aliyezifanya mbingu na nchi,

Bahari na vitu vyote vilivyomo.

(K) Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.


Huishika kweli milele,

Huwafanyia hukumu walioonewa,

Huwapa wenye njaa chakula;

Bwana hufungua waliofungwa;

(K) Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.


Bwana huwafumbua macho waliopofuka;

Bwana huwainua walioinama;

Bwana huwapenda wenye haki;

Bwana huwahifadhi wageni;

(K) Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.


INJILI

Mt 5:43-48

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,  ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies