NOVENA NI NINI

 


 Novena ni nini na ni ya nini?Novena (kutoka neno la Kilatini novem, 'tisa') ni zoezi la kujitolea ambalo hufanywa kwa siku tisa ili kupata neema au kuomba nia fulani. … Tofauti na oktava, ambazo ni za sikukuu kwa asili, novena hufanywa kwa nia au kumwombea mtu aliyekufa.

Novena ina maana gani kwa Wakatoliki?Novena ni aina ya maombi ya Kikatoliki ambayo unaweza kufanya kwa siku 9 au masaa 9. Ikiwa unaamua kuomba novena, lazima uombe sala maalum au mfululizo wa maombi na unataka katika akili. Novena inaweza kuwa sala yenye kuimarisha kiroho na inatumiwa sana na Kanisa Katoliki.

 SALA KABLA YA KUINGIA MFUNGO/NOVENA

Ee Mungu Baba mwenyezi uliyetufanya wanadamu kwa neema yako na ukataka tukurudie wewe kwa mioyo iliyotakata. Wewe ulisema sifurahi kifo cha mtu mwovu bali auache mwenendo wake mbaya apate kuishi. Ee Bwana wewe wajua kuwa hali yetu ya kibinadamu ni dhaifu, ndio maana ulituambia tubuni na kuiamini Injili. Mara kwa mara tunaahidi kuenenda katika uzima mpya kwa kukufuata wewe, lakini tena na tena tunajikuta tumeanguka dhambini kwa ajili ya ulegevu wa mwili. Badala ya kuichukua misalaba yetu na kumfuata Kristo, tunarudi nyuma na kuanguka tena dhambini. Uturehemu ee Bwana kwa ajili ya dhambi tunazozitenda.

Kwa maombezi ya Mt. Rita wa Kashia mama aliyesali sana, kufunga kwa muda mrefu, na kuutesa mwili wake, unisaidie niweze kufunga chakula na starehe, niache kutenda dhambi na furaha zilizozoea. Nijibidishe kutenda matendo ya huruma na kusali zaidi. Unipe ujasiri wa kuvumilia mateso na maumivu ya mwili yakayotokana na mfungo huu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies