ROZARI YA HURUMA YA MUNGU






JINSI YA KUSALI ROZARI YA HURUMA YA MUNGU

Tumia Rozari ya kawaida kusali Rozari ya Huruma ya Mungu kama ifuatavyo:
*Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu ....Amina*
*Anza kwa sala hii....*
Yesu, ulikufa, lakini chanzo cha uhai kilitoka kwa ajili ya watu, na bahari ya huruma ilifunguka kwa ajili ya ulimwengu mzima. Ee chemchemi ya Uhai, huruma ya Mungu isiyo na mwisho, ikafunika ulimwengu mzima na ukajimwaga mwenyewe juu yetu.
*BABA YETU.*
*SALAMU MARIA....X3*
*KANUNI YA IMANI.*

Kila penye punje kubwa (Badala ya Baba yetu):
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.
Kila penye punje ndogo (badala ya Salamu Maria):

MWANZISHAJI: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristu,
WOTE HUITIKIA: Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Mwisho wa Rozari sali sala ifuatayo mara tatu:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.

LITANIA YA HURUMA YA MUNGU.
Bwana utuhurumie –
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie – Kristo
utuhurumie
Bwana utuhurumie –
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie – Kristo
utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu –
utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia
Mungu - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu -
utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja –
utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu
ya Muumba wetu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha
ukamilifu wa Mwokozi wetu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo upendo
usiopimika wa Roho Mtakasa - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu fumbo
lisilofahamika la Utatu Mtakatifu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo ishara ya
uwezo mkuu wa Mungu
Mwenyezi - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu
iliyofumbuliwa katika kuziumba
Roho za Malaika wa mbinguni - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyotuumba
na kutuamuru tuwepo bila
kutokana na chochote - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayotujalia
maisha ya kutokufa - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayotukinga
na adhabu tunazostahili - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayotuinua
tutoke katika taabu, unyonge na
maumivu ya dhambi zetu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayotufanya
wenye haki katika Neno
aliyejifanya Mtu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayofurika
kutoka katika majeraha ya Kristo - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayobubujika
kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu
wa Yesu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyotupatia
Bikira Maria Mtukufu awe kwetu
Mama wa Huruma - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa
katika kuanzishwa Kanisa
Katoliki - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayopatikana
katika mafumbo ya Sakramenti
Takatifu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayotolewa
kwa wanadamu wote kwa njia ya
Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayotolewa
katika Sakramenti ya Ekaristi na
Upadrisho - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu
inayooneshwa kwetu pale
inapotuita na kutuingiza katika
kuwatakatifuza wenye haki - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayotimilika
katika ukamilifu wa watu
watakatifu - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu chemchemi ya
afya kwa wagonjwa na wote
wanaoteseka - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya
wote wenye uchungu moyoni - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo tumaini
la roho zinazosumbuliwa na
mkato wa tamaa - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi
wa daima na popote wa watu
wote - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu inayowahi
kutuletea neema zake - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo amani
yao wanaokufa - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo
burudisho na faraja yao
marehemu wa toharani - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo furaha
ya mbinguni kwa watakatifu wote - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu iliyo taji la
watakatifu wote - tunakutumainia.
Huruma ya Mungu chemchemi ya
miujiza isiyokauka - tunakutumainia.
Mwanakondoo wa Mungu
uliyetuonyesha huruma yako kuu
katika kuikomboa dunia kwa
msalaba wako mtakatifu -
utusamehe ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu
unayejitolea kwetu kwa mapendo
na huruma katika kila adhimisho
la Sadaka ya Misa Takatifu -
utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu
anayeondoa dhambi za dunia
kwa njia ya huruma yako isiyo
na mwisho - utuhurumie.
KIONGOZI: Bwana utuhurumie –
WOTE: Kristo utuhurumie.
KIONGOZI: Huruma anana za
Bwana zi juu ya kazi zake zote –
WOTE: Huruma za Bwana
nitaziimba milele.

TUOMBE: Ee Mungu uliye na
huruma isiyo na mwisho, na
hazina za wema na upendo wako
hazina mipaka. Tunakusihi
ututazame sisi watu wako huku
duniani na kutuongezea huruma
yako tena na tena, ili itusaidie
tusije tukakata tamaa hata mara
moja, haidhuru tukumbane na
majaribu makubwa kiasi gani,
bali tuweze daima kuzielekea na
kuzishika amri zako, kwa
matumaini na kutimiza mapenzi
yako matakatifu, ambayo ndiyo
huruma yenyewe. Tunaomba
hayo kwa njia ya Bwana wetu
Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa
Amani na Huruma, aishiye na
kutawala nawe, na Roho
Mtakatifu, kwa pamoja
mkituonyesha huruma, daima na milele.
Amina

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies