SALA YA KUWAOMBEA WATOTO WETU



SALA YA KUWAOMBEA WATOTO WETU.

Mungu Baba yetu, umetubariki sisi kwa zawadi ya Watoto, tunakushukuru kwa Lulu hizi za thamani zinazopamba nyumba yetu, kicheko chao kinatupatia sisi furaha na kuyang'arisha Maisha yetu, wenyewe ni Mwelezo wa uwepo wako katika nyumba yetu.
Kukua kwao kunaonyesha mafumbo ya upendo wako, wawezeshe kuonja uwepo wa upendo wako na kukomaa katika Hekima na kukua katika upendo wako, Maisha yajayo ya Watoto wetu yapo mikononi mwako, japokuwa nasi tuna jukumu katika kuelekeza mwelekeo wao wa baadae, tusaidie kuwa waaminifu katika jukumu letu ili kwamba tuweze kuwasaidia katika kuitikia Neema zako na hivyo wawe kama vile unavyotaka wawe.
Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies