VISAKRAMENTI NI NINI


Visakramenti ni nini?
Ni alama takatifu ambazo kwa sababu zinafanana na Sakramenti, zinaashiria kupatikana kwa matunda ya kiroho kupitia maombi ya kanisa. Visakramenti huwasaidia watu kupokea tunda la msingi la Sakramenti na mazingira mbalimbali ya maisha hutakaswa.

Katika maana nyengine: Visakramenti ni shara takatifu zilizoanzishwa na Kanisa ambazo lengo lake ni kuwaandaa watu kupokea tunda la Sakramenti na kutakatifuza mazingira mbalimbali ya maisha.
Mfano wa Visakramenti: Misalaba, Medani, Rozari, Skapulari, Maji ya baraka, Matawi yaliyobarikiwa, Majivu yaliyobarikiwa n.k


Visakramenti hufanyikaje?

Visakramenti hufanyika kwa njia ya Baraka. Ukiwa na Msalaba, Rozari Skapurari etc ambayo haijabarikiwa ni kazi bure haiweizi kufanya kazi yoyote. Ni baada ya kubarikiwa na Padre ndipo Visakramenti hupata pumzi ya uhai ndani yake. Hivyo twasema ni katika kubarikiwa Visakramenti hufanya hai navyo huweza kutubariki.


Kazi ya Visakramenti ni nini?

Visakramenti vinatutayarisha kupokea neema na pia kushirikiana nayo. Tofauti na Sakaramenti ambazo zenyewe hutoa neema. Hivyo huchota visakramenti nguvu kutoka katika Sakramenti. Chukua mfano wa Visakramenti tajwa hapo juu na angalia kazi yake, mfano Maji ya baraka au Rozari. Tafakari namna ambavyo Visakramenti vilivyobarikiwa vinavyotupa nafasi ya kuishi ukatoliki wetu.

Kwa uchache Visakramenti hutusaidia;

Kusali
Kutakari imani yetu
Kupinga pepo wabaya
Kupokea baraka mbalimbali
Kutukinga na hatari za kimwili na kiroho
Kubariki watu na vitu nakadhalika
Kuna kazi na faida nyingi tuzipatazo kutoka katika Visakramenti. Visakamenti ni mto wenye baraka tele ambao tunaweza kujichotea baraka tukienda na vyombo visafi.

Matumizi sahihi ya Visakramenti
Kuvaa

Visakramenti vimebarikiwa, hivyo ndani yake vimebeba baraka, ni muhimu vitumike kwa heshima kubwa sana. Ni busara kuvivaa wakati wote lakini si katika mazingira kama kumbi za starehe au disko au katika matendo ya uovu. Wawezaje kutenda dhambi huku umevaa Rozari au Skapulari?

Kuvitunza

Visakramenti kama Msalaba, Picha za watakatifu au maji ya baraka vihifadhiwe katika mahali pasafi na pa kupendeza, si vizuri kuvichnganya na vitu vengine. Maana hivi ni Vibarikiwa basi vitunzwe kama vibarikiwa.

Kusali

Hatuvai Visakramenti kama hirizi, tunahitaji vitusaidie kufikia Sakramenti mbalimbali. Tunapaswa kuvitumia katika sala sio kuviacha kama ulinzi tu, kama ni Rozari hakikisha unasali, kama ni msalaba upe heshima inayostahili.
Visakaramenti Vimeharibika Umbo/Unataka kuvitupa?
Visakramenti vyaweza kuharibika katika hali yake ya umbo, mfano Rozari imekatika, Picha imeungua nusu au msalaba umevunjika upande. Au ulikua na msalaba mdogo sasa umeninua mkubwa unataka kuutupa, je ni sahihi?

Tukumbuke visakramenti hufanyika katika ngazi mbili, kwanza umbo la halifi tunaloliona na pili Kubarikiwa kwake kunakofanya kuwa kisakramenti. Baraka huwa katika umbo zima si sehemu tu, hivyo kuharibika kwa umbo hakutoi baraka iliyomo ndani yake.

Visakramenti vinapoharibika twapaswa kuendelea kuvitunza kwa heshima kuu kama ambavyo tumevitunza kutoka awali. Kuvitupa au kuviharibu hii huwa ni kufuru kwa baraka iliyomo katika visakramenti. Kama hutaweza kuvitunza ni bora kuvipeleka kanisani nao watajua namna ya kuvihifadhi. VISAKRAMENTI HAVITUPWI.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies