FAHAMU KUHUSU SALA YA KANISA

 

Sala ya kanisa ni nini?
Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima

Vyanzo vya sala za Kikristo
Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu

Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?
Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu

Hekalu ndiyo nini?

Hekalu ndipo tunapomuendea Mungu kwa ibada. Vilevile sisi wenyewe ni Mahekalu.
Yesu aliheshimu na kutakasa hekalu pekee la taifa lake kama “nyumba ya Baba” yake (Yoh 2:16), lakini alitabiri kuwa litabomolewa moja kwa moja, na kuwa watu watapaswa kuabudu ndani yake aliye hekalu hai. “Wayahudi walisema, ‘Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?’ Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake” (Yoh 2:20-21).
“Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Ef 2:22).
“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi” (1Kor 3:16-17).

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies