JE WAJUWA KWAMBA MWEZI HUU AGOSTI NI MWEZI WA KUOMBEA AKINA MAMA KWENYE NDOA NA MAHUSIANO?_*


🟤🟤Mwezi huu wa Nane ni mwezi wa Mt. MONICA hivyo kama una hitaji kuomba juu ya ndoa yako Msogelee MUNGU kupitia maombezi ya Mt. MONICA
🟤🟤Tunaungana nawe kukuombea wewe mwenye uchungu mzito utokanao na maumivu katika ndoa yako
🟤🟤Mwezi huu tutaomba pamoja na wewe ambaye moyo wako umeinama chini kwa sababu ya makwazo mbalimbali
🟤🟤Tutaomba nawe wewe ambaye huyo mwenza wako kun wakati anakuweka njiapanda juu ya mambo fulani
🟤🟤Tutakuombea wewe mama ambaye umebebeshwa roho ya kukataliwa na upande mmoja wa ndugu wa mwanandoa wako ili Mungu akaachilia kibali cha kukubaliwa yote haya yatawezekana kwa msaada wa Muombezi wa ndoa na Mahusiano Mt. MONICA
🟤🟤Pia tutasema na Mungu kwa kumwinamia na kumnyenyekea aachilia uzao kwa watu wake ambao wamebeba aibu ya miaka mingi kwa kutopata watoto
🟤🟤Kama ndoa yako imebeba sehemu kubwa ya malalamishi yaani kila ukifanya hili hata kama ni Zurich bado tu unabebeshwa lawama...hali hii huuma sana sana bila msaada wa Mungu hakika hatuwezi songa mbele
🟤🟤Kwanini uendelee kuwalilia wanadamu wenzako kwa sababu ya mahusiano ama ndoa? Hamishia machozi yako kwa Bwana kwa kumwambia inatosha Bwana
🟤🟤Tunawaombea pia Akina mama wore Wajawazito Mungu aendelee kuwa nyumba salama ya kuishi watoto walioko matumboni mwenu
🟤🟤Mimba zote zenye kuambatana na changamoto yeyote ..Mungu akaachilie uponyaji na furaha wakati wa kuwaleo hawa watoto wakiwa matumboni
🟤🟤Tunaomba pia maombi haya yakaambatane na kuwatoa hofu akina Mama wote wajawazito kwa kuamini kwamba Mungu atawasimamia salama mpaka siku ya kujifungua
🟤🟤Tutaziombea pia ndoa zote zenye changamoto mbali ili zikastawi upya
🟤🟤Vikwazo vyote ambavyo huwa vinajiyokeza wakati ikianza mikakati ya kuzibariki ndoa ambazo hazijabarikiwa zikaweze kufunguka
🟤🟤Kwa imani Mungu ataenda kusimama na wewe Mama/Baba unayejiona umedhurumiwa haki yako ya upendo
🟤🟤Mungu akewe sababu ya kuanza upendo mpya kwenye ndoa ama mahusiano yako mpendwa
🟤🟤Kwa imani mwezi huu wa Agosti utakuwa ni mwezi wa kipekee kwa kuachilia msamaha wa kweli kabisa
🟤🟤Mungu wa Mbinguni akaipokee sala yako mbele za ifalme wake na kukuweka katika viwango vya juu zaidi
*Zaburi 141:2*
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
MTAKATIFU MONICA NA WATAKATIFU WOTE WA MUNGU MTUOMBEE

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies