KANISA KATOLIKI NI NINI

 












Kanisa Katoliki ni nini?
Kanisa Katoliki ndio Jumuia ya Wakristu Wote pamoja na Maaskofu na Mapadri wanaoshiriki imani moja chini ya Baba Mtakatifu Mkuu wao.
Alama za kanisa la kweli ni zipi?

Alama za kanisa la kweli ni hizi;
1. Kanisa ni moja
2. Kanisa ni Takatifu
3. Kanisa ni Katoliki
4. Kanisa ni la Kitume
5. Kanisa ni la Kimisionari

Ni nani ameanzisha Kanisa Katoliki?
Yesu Kristo ameanzisha Kanisa Katoliki

Jimbo Katoliki ni nini?
Jimbo Katoliki ni Jumuiya ya Wakristo ambao katika Imani na Sakramenti wana ushirika na Askofu aliye halifa wa Mitume.
Yesu aliweka makanisa mangapi? Yesu hakufanya makanisa mengi?
Hapana. Yesu alifanya Kanisa moja tuu.
Mungu ni Mmoja muumba na Baba wa wote, Mkombozi ni mmoja tuu, Yesu Kristo, Dini ni moja, Imani ni moja, Ubatizo ni mmoja, basi Kanisa ni moja kwa watu wote na nchi zote.

Kwa kusudi gani Yesu alianzisha Kanisa?

Yesu alianzisha Kanisa kwa nia ya Kuutangaza na kuueneza Ufalme wa Mungu (Mt 28:19-20)
Kanisa linatimiza kusudi la Yesu Kristo kwa namna gani?

Kanisa linatimiza kusudi la Yesu Kristo kwa;
1. Kwa Ualimu wake yaani kuwafundisha watu
2. Kwa Ukuhani wake yaani kuwatakasa watu
3. Kwa Uchungaji wake yaani kuwaongoza watu.

Kanisa ni Moja maana yake ni nini?
Kanisa ni moja maana yake ni la mahali popote na siku zote lina mafundisho yale yale, Sakramenti zile zile na mkubwa mmoja.

Kanisa ni Takatifu maana yake ni nini?

Kanisa ni Takatifu maana yake:-
1. Limeanzishwa na Mungu mwenyewe aliye Mtakatifu
2. Kristo aliye Mtakatifu alijitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake ili kulitakasa
3. Roho Mtakatifu hulihuisha kwa upendo wake
4. Ndani yake wamo Bikira Maria na Watakatifu wengi wanaoliombea

Kanisa ni Katoliki maana yake ni nini?
Kanisa ni Katoliki maana yake ni la watu wote mahali pote na nyakati zote.

Kanisa ni la Kitume maana yake ni nini?
Kanisa ni la Kitume maana yake wakubwa wake yaani Baba Mtakatifu na Maaskofu nimahalifa wa Mitume

Kanisa ni la Kimisionari maana yake ni nini?
Kanisa ni la Kimisionari maana yake limetumwa kupeleka habari njema kwa mataifa yote. (Mt 28:19-20)



No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies