KWA NINI TUNAMUOMBA MAMA BIKIRA MARIA

 

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.
Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?
Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Mama wa Yesu ni nani?
Mama wa Yesu Kristo ni Bikira Maria.
“Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 28Naye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!” 29Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” 30Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” 34Maria akamwuliza huyo malaika, “Maadam mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” 35Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu Zake Yeye Aliye Juu zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 36Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 37Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”(Lk 1:26-37).
Yesu ni Mungu ndio maana Bikira Maria akaitwa Mama wa Mungu kwa sababu ndiye aliyemzaa Yesu. Yaani Bikira Maria ni Mama wa Mungu tuu kwa sababu ya kumleta Yesu Duniani kama mzazi wa kimwili.
Hii haimaanishi kwamba Bikira Maria ni Mama wa Yesu kabla ya Yesu kuja Duniani kwa maana Yesu Alikuawepo kabla ya kuzaliwa kwake.

Bikira maria anamwita Yesu Mwanae wa kumzaa na vilevile anamwita Bwana na Mungu wake kwa kuwa ni Mungu wake pia na hivyo ni mdogo mbele ya Yesu. Sisi tunapomuita Bikira Maria Mama wa Mungu tunaheshimu nafasi yake ya kipekee ya kuizalia Dunia Yesu aliye Mungu. Kwa kuwa Bikira Maria ni Mdogo kuliko Mungu na Hana Umungu wowote hivyo haabudiwi kama Mungu au pamoja na Mungu.
Tunamuheshemu tuu Bikira Maria na Kumuomba atuombee kwa Mungu mwanaye 
Bikira Maria anafaida yeyote kwa Kanisa?Ndiyo. Bikira Maria ni mwombezi Mkuu wa Kanisa. kwa sababu anayo nafasi ya kipekee mbele ya Mungu mwanaye Yesu kama Mama yake wa kumzaa Duniani na kama mlezi wake akiwa duniani tangu kuzaliwa mpaka kufa Msalabani wakiwa pamoja.

Hapa duniani Yesu alizaliwa na nani?
Hapa duniani Yesu alizaliwa na Bikira Maria kama malaika alivyomuambia:
“Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo, hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu” (Lk 1:35).
( Hide )

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies