Kwanini Wakatoliki mnaungama dhambi kwa padre ?



KWANINI WAKATOLIKI MNAUNGAMA DHAMBI KWA PADRE AMBAYE NI MWANADAMU NA MDHAMBI BADALA YA KUUNGAMA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU?


Hapa tunaongozwa na maneno ya Bwana Yesu mwenyewe alipotoa amri hiyo kwa mitume wake akisema;
“Pokeeni Roho Mtakatifu.wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa na wowote mtakaowafungia dhambi wamefungiwa”(Yohane 20:22-23).
Na huo ndio utaratibu wetu tangu mwanzo wa kanisa la mitume.
“Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa”(Yakobo 5:16a)
Ni miongoni mwa maagizo msingi kabisa ambayo hatuna mamlaka kuyabadili labda Yesu mwenyewe aliyeagiza hivyo aje mwenyewe kuyabadilisha.
Mungu anayesamehe dhambi ndiye aliyechagua njia ya kutoa msamaha huo,sisi tu nani tumpange njia ya kutoa msamaha huo na kujipangia njia zetu?je tunamfundisha Mungu kazi?
Inashangaza siku hizi kusikia kwamba hata baadhi ya wakatoliki wameanguka katika mtego huu wa kutaka kubadilisha agizo hili la Yesu na inashangaza ni kwanini wanataka kurahisisha mambo kiasi hicho.

Mungu hafanyi kazi zake hewani bali huzifanya kupitia kwa watu wake.
Tunapoomba msamaha tunategemea kusikia maneno kama vile “nimekusamehe”,hutaka kuamini kwamba mtu akinyamaza au akiongea kimoyomoyo basi amekusamehe.
Yesu kwa kujua umuhimu na kazi ya neno hilo,alilitumia yeye mwenyewe akiwa binadamu(Luka 7:48).
Luka 7:48

“Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,umesamehewa dhambi zako”
na alitaka aendelee kulitumia hata utimilifu wa dahari katika hali ya kibinadamu,ndio maana aliwaachia binadamu baada ya kifo chake ili waendeleze kazi hiyo.
Kuondolea watu dhambi ni moja ya utume wa Yesu(Marko 2:10),ni pamoja na kazi hiyo aliwaachia mitume wake(Yohane 20:23).
Tukilinganisha na mfano wa mtume Petro baada ya kumkana Bwana,tunaweza kujifunza kwamba tunapoongea na Mungu peke yetu ni katika hali ya toba na majuto(Luka 22:61-62).
Luka 22:61-62
“Bwana akageuka na kumtazama Petro,naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana ‘leo kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu’ hapo akatoka nje,akalia sana.”
Hivyo bado tunadaiwa kuungama ili kuondolewa dhambi zetu(Yohane 21:15-17)

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies