LITANIA YA JINA TAKATIFU LA YESU

LITANIA YA JINA TAKATIFU LA YESU

Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Kristo utuhurumie.
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie.
Kristo utusikie
Kristo utusikilize.
Mungu, Baba wa mbinguni Utuhurumie
Mungu Mwana, Mkombozi wa dunia Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja Utuhurumie
Yesu, Mwana wa Mungu mzima Utuhurumie
Yesu, ung’aro wa Baba Utuhurumie
Yesu, nuru ya mwanga wa milele Utuhurumie
Yesu, mfalme wa utukufu Utuhurumie
Yesu, jua la haki Utuhurumie
Yesu, Mwana wa Bikira Maria Utuhurumie
Yesu, mpendelevu Utuhurumie
Yeau, mstaajabivu Utuhurumie

Yesu Mungu mwenye nguvu Utuhurumie
Yesu, Baba wa uzima ujao Utuhurumie
Yesu, Mjumbe wa shauri kuu Utuhurumie
Yesu, mwezaji Utuhurumie
Yesu, mvumilivu Utuhurumie
Yesu, mtii Utuhurumie
Yesu, mwenye moyo mpole na mnyenyekevu Utuhurumie
Yesu, mwenye kupenda usafi Utuhurumie
Yesu, mwenye kutupenda sisi Utuhurumie
Yesu, Mungu wa amani Utuhurumie

Yesu asili ya uzima Utuhurumie
Yesu, mfano wa fadhila Utuhurumie
Yesu, mwenye juhudi na roho za watu Utuhurumie
Yesu, Mungu wetu Utuhurumie
Yesu, makimbilio yetu Utuhurumie

Yesu, Baba wa maskini Utuhurumie
Yesu, hazina ya waumini Utuhurumie
Yesu, mchungaji mwema Utuhurumie
Yesu, mwanga wa kweli Utuhurumie
Yesu, hekima ya milele Utuhurumie

Yesu, wema usio na mwisho Utuhurumie
Yesu, njia na uzima wetu Utuhurumie
Yesu, furaha ya Malaika Utuhurumie
Yesu, Mfalme wa Mababu Utuhurumie
Yesu, Bwana wa Mitume Utuhurumie

Yesu, mwalimu wa Waenjili Utuhurumie
Yesu, nguvu ya Mashahidi Utuhurumie
Yesu, mwanga wa Waungama Utuhurumie
Yesu, usfi wa Mabikira Utuhurumie
Yesu, taji la Watakatifu Utuhurumie

Utuhurumie Utusamehe Yesu
Utuhurumie Utusikilize Yesu

Katika uovu wowote Utuopoe Yesu
Katika dhambi yoyote Utuopoe Yesu
Katika hasira yako Utuopoe Yesu
Katika mitego ya shetani Utuopoe Yesu
Katika tama ya uchafu Utuopoe Yesu
Katika mauti ya milele Utuopoe Yesu

Katika kudharau mashauri yako Utuopoe Yesu
Katika fumbo la kujifanya mtu Utuopoe Yesu
Kwa kuzaliwa kwako Utuopoe Yesu
Kwa utoto wako Utuopoe Yesu
Kwa maisha yako ya kimungu Utuopoe Yesu
Kwa kazi yako Utuopoe Yesu

Kwa maumivu ya mateso yako Utuopoe Yesu
Kwa msalaba na ukiwa wako Utuopoe Yesu
Kwa udhaifu wako Utuopoe Yesu
Kwa kufa na kuzikwa kwako Utuopoe Yesu
Kwa kufufuka kwako Utuopoe Yesu
Kwa kupaa kwako mbinguni Utuopoe Yesu
Kwa kuweka kwako Ekaristi Takatifu Utuopoe Yesu
Kwa furaha zako Utuopoe Yesu
Kwa utukufu wako Utuopoe Yesu

Mwanakondo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Utusamehe, Yesu.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Utusikilize, Yesu.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Utuhurumie, Yesu.
Yesu utusikie
Yesu utusikilize.

Tuombe:

Ee Bwana Yesu Kristo uliyesema:Ombeni mtapewa, tafuteni mtapata, pigeni hodi mtafunguliwa. Twakuomba utujalie sisi tujae mioyoni mwetu mapendo yako ya kimungu.Tupate kukupenda kwa moyo wote, kwa maneno na matendo, wala tusiache kamwe kukusifu.
Ee Bwana, utujallie daima uchaji na upendo, kwa jina lako takatifu, kwaa maana huwanyimi kamwe ulinzi wako hao uliowaimarisha katika upendo wako. Unayeishi na kutawala, milele. Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies