LITANIA ZA MOYO WA YESU

LITANIA ZA MOYO WA YESU

Bwana utuhurumie . Bwana utuhurumie.

Kristo utuhurumie . Kristo utuhurumie.

Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie.

Kristo utusikie. Kristo utusikilize.

Baba wa mbingu, Mungu, utuhurumie

Mwana, Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.

Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.

Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, Mwana wa Baba wa
Milele, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, uliotungwa na Roho Mtakatifu

Mwilini mwa Mama Bikira, utuhurumie

Moyo wa Yesu, ulioungana na Neno wa Mungu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, ulio na utukufu pasipo mfano, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, hekalu takatifu la Mungu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, hema la Yule Aliye juu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, nyumba ya Mungu na mlango wa mbinguni, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, tanuru yenye kuwaka mapendo, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, chombo cha haki na upendo, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, unaojaa upendo na wema, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, kilindi cha fadhila zote, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, unaostahili sifa zote, utuhurumie.

Moyo wa yesu, unaotawala mioyo yote, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, zinamokaa hazina za hekima na elimu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, mnamokuwa utimilifu wote wa Mungu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, uliopendelewa kabisa na Mungu Baba, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, uliotueneza maziada yake, utuhurumie.

Moyo wa Yesu

Mtamaniwa wa vilima vya milele, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, wenye uvumilivu, na huruma nyingi, utuhurumie.

Moyo wa Yesu,tajiri kwa wote wenye kukuomba, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, chemchemi za uzima na utakatifu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu,malipo kwa dhambi zetu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, ulioshibishwa matusi, utuhurumie.

Moyo wa Yesu,uliovunjika kwa sababu ya ubaya wetu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, uliotii mpaka kufa, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, uliochomwa kwa mkuki, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, chemchemi ya faraja zote, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, uzima na ufufuo wetu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, amani na upatanisho wetu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, sadaka ya wakosefu, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, mnamokuwa wokovu wao utuhurumie.

wenye kukutumainia, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, matumaini yao wenye kuzimia kwako, utuhurumie.

Moyo wa Yesu, sababu ya furaha kwa Watakatifu wote, utuhurumie.



Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za ulimwengu, utuhurumie. (mara tatu)Yesu, mwenye Moyo mpole na mnyenyekevu,
Uzilinganishe nyonyo zetu na moyo wako.



Tuombe. Ee Mungu, mwenyezi wa milele, uuangalie Moyo wa mwanao mpendelevu, pia na heshima na malipo aliyokutolea kwa ajili ya wenye dhambi, uridhike, uwaondolee wenye kuomba toba kwako kwa njia ya huyo Mwanao Yesu Kristo, anayeishi na kutawala nawe pamoja na Roho Mtakatifu, Mungu, milele na milele. Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies