MASOMO YA MISA, ALHAMISI, 17 AGOSTI, 2023


SOMO 1


Yos 3: 7-11, 13-17


Bwana alimwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa. Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani.

Basi Yoshua akawaambia wanu Israeli, Njoni huku, mkayasikie maneno ya Bwana, Mungu wenu. Yoshua akasema, kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi. Tazama, sanduku la agano la Bwana wa dunia yote linavuka mbele yenu na kuingia Yordani. Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukao sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu.

Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno,) ndipo hayo maji yaiiyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko. Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana wakasikamama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 114 :1-6

Aleluya.
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.

(K) Aleluya

Bahari iliona ikakimbia,

Yordani ilirudishwa nyuma.

Milima iliruka kama kondoo waume.

Vilima kama wana-kondoo.

(K) Aleluya.

Ee bahari, una nini, ukimbie?

Yordani, urudi nyuma?

Enyi milima, mruke kama kondoo waume?

Enyi vilima, kama wana-kondoo?

(K) Aleluya.

SHANGILIO
Efe 1: 17, 18


Aleluya, aleluya,
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristu,
awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.

Aleluya
.
INJILI
Mt. 18:21 - 19:1


Petro alimwendea Yesu akamwambia, Bwana, ndugu vangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini
Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiw’aye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhu- rumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.
Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. I.akini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.
Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akamneleka kwa watesaii, hata atakapoilipa deni ile yote.
Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyo- watenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake. Ikawa Yesu alipomaliza maneno havo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng’ambo ya Yordani.


No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies