MASOMO YA MISA ,JUMAMOSI,26 AGUST ,2023

MASOMO YA MISA JUMAMOSI


SOMO 1
Rut. 2:1-3, 8-11; 4:13-17

Naomi alikuwa na ndugu ya mumewe, mtu mkuu mwenye mali, wa jamaa yake Elimeleki, na jina lake aliitwa Boazi.

Naye Ruthu Mmoabi akamwambia Naomi, Sasa niende kondeni, niokote masazo ya masuke nyuma yake yule ambaye nitaona kibali machoni pake. Akamwambia, Haya, mwanangu, nenda. Basi akaenda, akaja akaokota masazo kondeni nyumba ya wavunaji; na bahati yake ikamtukia kwamba akaifika sehemu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.

Basi Boazi akamwambia Ruthu, Mwanangu, sikiliza; wewe usiende kuokota masazo katika shamba liongine, wala usiondoke hapa, lakini papa hapa karibu na wasichana wangu. Macho yako na yaelekee konde walivunalo, ufuatane nao; je! Sikuwaagiza vijana wasikuse? Tena, ukiona kiu, uende kwenye vyombo, nawe uyanywe waliyotenda hao vijana. Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani nimepata kibali machozi pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni? Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukafikilia watu usiowajua tangu hapo.

Basi Boazi akamtwaa ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake; na Bwana akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa motto wa kiume. Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe Bwana, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli. Naye atakurejezea uhai wako, na ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake.

Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.


WIMBO WA KATIKATI

Zab. 128:1 – 5

Heri kila mtu amchaye Bwana,

Aendaye katika njia yake.

Taabu ya mikono yako hakika utaila;

Utakuwa heri, na kwako kwema.

(K) Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.


Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,

Vyumbani mwa nyumba yako.

Wanao kama miche ya mizeituni

Wakiizunguka meza yako.

(K) Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.


Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.

Bwana akubariki toka Sayuni;

Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako.

(K) Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.


SHANGILIO
Zab. 119:28, 33

Aleluya, aleluya,

Unitie nguvu sawasa na neno lako, ee Bwana,

unifundishe njia ya amri zako.

Aleluya.


INJILI
Mt. 23: 1-12

Yesu aliwambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yoyote watakayowaambia, myashike, na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.

Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies