SALA ZA JIONI



SALA YA JIONI.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.
Tunakushukuru ee Mungu kwa mema yote uliyotujalia sikuu hii ya leo.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salam Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
SALA YA IMANI.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
UNGAMO LA DHAMBI.
Na tuwaze katika moyo makoda yote ya leo tuliyomkosea Mungu, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo(………………………)
Namuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutokutimiza wajibu, nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria mwenyeheri, Bikira daima, malaika na watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
+Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu na atufukishe kwenye uzima wa milele, Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu, nimetubu sana niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi. Amina.
Ee Mungu mwenye huruma, uwashushie baraka zako, Baba Mtakatifu wetu Francis na maaskofu, na mapadre, na mashemasi, wakulima, wafanyakazi wote, wanafunzi na jamii yote unaowafanya kuwa watu wako . Uwaokoe washenzi, uwafariji wagonjwa, waelekee wanaozimia waweze kuona mwanga wa milel, Amina.
ANGELUS.
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria,naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Ndimi mtumishi wa Bwana,nitendewe ulivyosema.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Neno wa Mungu akatwaa mwili,akakaa kwetu.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Utuombee mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika, kwamba Kristo mwanao amejifanya mtu; kwa mateso na msalaba wake, tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Bikira Maria Malkia wa amani~Utuombee!
SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies