Tanzania,Tamko la TEC kuhusu Mkataba wa bandari:Raia wasikilizwe na Serikali!

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Ijumaa tarehe 18 Agosti 2023 limetoa tamko kuhusu mkataba kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Falme za nchi Uarabuni,Dubai kuhusiana na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa mendeleo na uboreshaji wa bandari za Bahari na za maziwa Tanzania.Ushauri "Serikali isipuuze sauti ya wananchi."

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ijumaa tarehe 18 Agosti 2023, Baraza la Maaskofu Katoliki Nchini Tanzania (TEC) limetoa tamko la kupinga mkataba wa usimamizi na uendelezaji wa bandari za Nchi uliosainiwa kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Nchi za Falme za Uarabuni huko Dubai na kuridhiwa kupitia azimo la Bunge mnamo tarehe 10 Juni 2023, huku wakifafanua kwa kina jinsi ambavyo mkataba huo haukubaliki kwa watanzania wengi, tangu kuanza kwa mjadala. Tamko hilo limesainiwa na Maaskofu wakuu na maaskofu wote 37 wa Majimbo Katoliki Tanzania ambapo kabla ya kukabidhiwa kwa Mkataba huo kwa waandishi wa Habari, imetangazwa kwa umma na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mheshimiwa Padre Charles Kitima kwa vyombo vya Habari

MAASKOFU KATOLIKI WA TANZANIA

Kwa upande wake Padre Kitima amesema Maaskofu hawaungi mkono bandari kuwekwa chini ya mwekezaji mmoja na kwamba tamko hilo la Maaskofu lina kauli moja ambayo ni kwamba “kama wananchi hawautaki mkataba, serikali iwasikilize wananchi. Serikali iachane na Mkataba wa Bandari kwa sababu wananchi wamegawanyika kuhusu mkataba huo na zaidi ni kutokana na vifungu flani fulani ambavyo haviendani na Katiba ya Nchi na matakwa ya raia”. Hata hivyo hii siyo kwa mara ya kwanza sauti ya Viongozi wa kidini kusikika, hata siku zilizopita waliweza kutoa maoni yao na sio viongozi wakatoliki tu, lakini hata wa makanisa mengine na madhehebu mbali mbali kupitia mijadala.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies