DIVAI ILIYOTUMIWA NA YESU ILIKUWA NA KILEVI?



Divai iliyotumiwa na Yesu ilikua na Kilevi (pombe)?
Ndiyo, Divai aliyoitumia Yesu kuigeuza kuwa damu yake ilikua na kilevi kwa sababu kwa kawaida kipindi cha Pasaka sio msimu wa kuvuna zabibu na hakukuwa na njia yoyote ya kufanya juisi yake isiwe kilevi. Kwa hiyo hakukuwa na uwezekano wa kupata juisi ya zabibu isipokua mvinyo wa zabibu wenye kilevi. Vile vile Wayahudi walikua na desturi ya kutumia Mvinyo wa zabibu kama kinywaji cha sikukuu ya pasaka.
Hakuna sehemu kwenye Bilia tunaambiwa kwamba ulifanyika Muujiza wa Kufanya Divai isiwe kilevi. Biblia inatuambia kuwa Mitume kila walipokutana Walishiriki Meza ya Bwana. Haikutuambia walishiriki meza ya Bwana tuu Kipindi cha kukamua Zabibu.
Biblia inatuthibitishia kuwa Divai aliyotumia Yesu na Mitume ilikua na kilevi kwa kusema kuwa wengine walikuwa wakilewa katika Meza ya Bwana (Wakorinto 11:22).
Biblia haituambii kuwa Yesu alitumia Divai isiyo na kilevi. Wala Yesu hakuwahi kuonya kuhusu kutumia Divai yenye Kilevi. Yesu katika Umungu wake angeweza kujua kuwa miaka ijayo Divai ambayo ingetumika ingekuwa na Kilevi kwa hiyo angeonya Matumizi yake.
Divai iliyotumiwa na Yesu na Mitume ilikua na Kilevi ndio maana Mitume waliwaonya wakristo wa kwanza juu ya ya kushiriki vibaya Meza ya Bwana mfano kulewa kama tunavyosoma kwenye mistari ifuatayo.
17Basi katika maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu, kwa sababu mkutanikapo si kwa ajili ya faida bali kwa hasara. 18Kwanza, mnapokutana kama kanisa, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo. 19Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili kuonyesha ni nani anayekubaliwa na Mungu. 20Mkutanikapo pamoja si chakula cha Bwana mnachokula, 21kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine, huyu hukaa njaa na mwingine analewa. 22Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha! 23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema “Huu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.” 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. 31Lakini kama tungejipambanua wenyewe tusingehukumiwa. 32Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadabishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane. 34Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani kwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa. Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.(Wakorinto 11:17-29)
Kwa hiyo hata Mitume na Wakristu wa kwanza walitumia divai yenye kilevi kwenye Meza ya Bwana (Ekaristi) ndio maana kuna waliolewa.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies