TAFAKARI YA JUMAMOSI SEPTEMBER 23,2023















Jumamosi, Septemba 23, 2023
Juma la 24 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Padre Pio wa Pietrelcina
1 Tim 6: 13-16;
Zab 99: 1-5;
Lk 8: 4-15

KUMSIKILIZA MUNGU!
Somo la Injili linatueleza leo kuhusu mfano wa mpanzi na kufuatwa na maana yake. Mbegu inaoneshwa kama Neno la Mungu, wale walio pembezoni mwa barabara ni wale wanaosikia na yule muovu huja na kulichukua neno kutoka ndani ya mioyo yao, ili wasiweze kuamini.

Mfano huu hunyambulisha njia nne ambazo tunasikia neno la Mungu . Wengine wapo kama njia, wengine kama mwamba, wengine kama udongo uliosongwa na miiba, na wengine kama udongo mzuri. Kama mfano wa haya yote kuna uwezekano wa kukuwa kwa neno la Mungu. Udongo mzuri ni pale ambapo neno la Mungu linapokelewa na kuzaa matunda. Mbegu iliyosongwa na miiba ni pale ambapo neno la Mungu linakuwa lakini matunda yanaondolewa na matatizo ya kila siku na vishawishi. Hizi mbegu zilizo anguka kwenye mwamba hukuwa lakini pale maisha yanapo kuwa magumu hukauka na kuacha kutoa matunda. Mbegu za kwanza kuanguka njiani, ni za mwisho kabisa kutamanika kati ya zote. Katika hali hii hata mbegu zenyewe hazikui. Ardhi inafanywa ngumu kiasi kwamba hata haziwezi kuzama ndani. Hata njia yenyewe haiwezi kuleta mazingira mazuri kuiruhusu kuota, na kama Injili inavyosema, yule muovu huja nakuiiba ile mbegu hata kabla haijakuwa.

Tafakari njia mbali mbali ambapo shetani anaweza kuja na kuliiba lile neno la Mungu ndani yako. Inaweza kuwa katika hali ya kukuweka wewe na mambo mengi sana kiasi ambacho hupati muda kabisa wa kuzamisha neno la Mungu ndani mwako. Au inaweza kuwa ni katika hali ya kuruhusu kelele za ulimwengu zikusumbue na kulisonga lile neno na kushindwa kuliacha lizame ndani. Bila kujali upo katika hali ghani, kilicho cha muhimu ni kutengeneza mazingira mazuri ya kulisikiliza neno la Mungu na kulielewa. Hatua hiyo ya kwanza inapo fanikiwa unaweza sasa ukaondoa, miamba na miiba kutoka katika udongo wa roho yako.

Sala: Bwana, nisaidie niweze kusikiliza neno lako, nilisikilize, kulielewaa na kuliamini. Nisaidie moyo wangu uweze kuwa udongo mzuri ili liweze kuingia na kuzaa matunda mema. Yesu nakuamini wewe. Amina

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies