TAFAKARI YA MASOMO YA MISA 28,SEPTEMBER


Tafakari ya masomo ya Misa 28 September
Hagai anatumwa na Mungu kwa taifa
lake kuwafanulia chanzo cha matatizo
yao. Kwamba walikuwa wamepuuzia
nyumba ya Mungu kwamba sio wakati
wa kuirekebisha. Wanaishi kwenye
nyumba nzuri ila nyumba ya Mungu
ikiharibika. Anawaalika kutafakari
madhara ya kupuuza kazi ya Mungu,
wanapanda mbegu nyingi na kuvuna
kidogo, wanakula lakini hawashibi,
wanakunywa lakini hawaridhiki.

Anawaalika kutathmini maisha yao,
kuanza upya kwa kulijali kanisa la
Mungu na kulijenga. Anawaelekeza
kutafakari dhamiri zao ili kuzijutia
na kufuata njia iliyo sahihi. Waumini
wanapaswa kulitegemeza kanisa la
Mungu kwa kila namna. Sio halali
kuishi kwenye nyumba ya fahari na
starehe huku huduma Mungu. Tutumia
raslimali zetu katika kulijenga kanisa
la Mungu, ili nasi tufaidi jasho letu na
miradi yetu iweze kufanikiwa. Nguvu
zetu na kazi zetu zitumike kulisaidia
kanisa la Mungu kuenea na sio kuwa
kikwazo cha uinjilishaji.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies