TAFAKARI YA MASOMO YA MISA JUMATANO 20;SEPTEMBA

1 Kor 12:31 – 13:13;
Zab 32: 2-5, 12, 22;
Lk 7: 31-35.

KUFUNGUA MIOYO YETU KWA YESU
Kwenye somo la injili Yesu anakishangaa kizazi hiki kwani kinachezewa ngoma, kinaambiwa kifanye jambo hili lakini basi hakifuati. Kina ukaidi mkubwa na ukosefu wa upendo na hivyo basi kimeshindwa kutambua na kusoma alama za ulimwengu. Hii yote ni kwa sababu kilikosa upendo na kuwa na majivuno. Kikaona watu kama akina Yohane Mbatizaji na Yesu kama vituko tu. Kilitaka mawazo na mipango yao ifuate hali ya kuachana na wengine.

Sisi tuachane na mawazo kama haya ya hiki kizazi kwa kuwa watu wenye upendo zaidi, mshikamano na kuacha majivuno. Majivuno yametufanya tusiwe wa faida ndani ya ulimwengu.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies