TAFAKARI YA MASOMO YA MISA SEPTEMBER;30 ,2023

Tafakari ya masomo ya Misa 30 September

Taifa la Mungu
linatangaziwa kuwa, hata kama
halina uzio kwa usalama wake,
Mungu mwenyewe ataulinda kwa
kuta za moto, hivi kwamba hakuna
adui yeyote atakayeushambulia.

Yerusalemu inafurahia ulinzi kamili
kwa ajili ya ukombozi wa watu wake.
Kweli Bwana asipoulinda mji mlinzi
anafanya kazi bure. Taifa la Mungu
baada ya kujitahidi kuishi kwa kuyatii
maagizo yake, lilifurahia ulinzi wake.

Katika injili Yesu anatangaza kukaribia
kuteswa kwake kwa ajili ya kutoa
nafsi yake kama fidia ya wokovu wa
mwanadamu. Lakini anawahimiza
kuyashika maneno yake. Sawa na
Mungu anavyolijali na kulitunza taifa
lake, vivyo hivyo na Kristo analijali
na kulitunza kanisa lake. Taifa lolote
linapomtumainia Mungu na kutenda
yanayofaa, linakuwa na uhakika
wa uridhi wake, hata kama halina
nguvu ya kujilinda lenyewe. Waumini
wana usalama na matumaini ya
heri, kutokana na Ukombozi wa
Bwana Yesu Msalabani. Inatulazimu
kumshukuru Mungu kila wakati na
kuomba msaada wa ulinzi wake.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies