TAFAKARI YA MOSOMO YA MISA SEPTEMBER 27,2023

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA 27;SEPTEMBER
YOTE NI KWA NEEMA ZA MUNGU:

Nabii Ezra anaonyesha umahiri wake
katika sala na mawasiliano yake
na Mungu. Ananyenyekea mbele
za Mungu, na kutambua rehema za
Mungu alizowajalia taifa la lsraeli.
Anatambua kwamba walikuwa
watumwa chini ya Ufalme wa Babiloni,
hadi Mungu alipowarehemu nĂ 
kuwafanya tena kuwa huru chini ya
Ufalme wa Uajemi. Anatambua pia
nguvu ya Mungu iliyowaunganisha na
kuwapa nguvu hadi kusimamisha tena

Hekalu la Yerusalemu. Hapo ndipo
anapowasilisha ombi lake la kujaliwa
Yerusalemu kujenga ukuta. Waumini
wajifunze kunyenyekea na kutambua

neema za Munau katika maisha
yao, kabla ya kutoa sala zao. Kanisa
pia liuone mkono wa Mungu katika
kuendelea kwake, na lijitahidi kuwa
mfano bora wa kumtukuza Mungu
kwa kufanikiwa kustahimili nyakati
ngumu. Sawa na maneno ya Kristo
kwa Mitume wake. Tujifunze wote
kutegemea neema za Mungu katika
kazi ya uinjilishaji.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies