UBANI NI NINI

FAHAMU KUHUSU UBANI
\
Katika Agano la kale Mungu aliwaamuru au kuwaagiza watu wake kuchoma Ubani rejea kitabu cha kutoka 30:7 na 40:27.
Wapendwa katika Bwana, UBANI (Uvumba) hutumika katika Kusifu,Kubariki na Kutakatifuza Matakatifu na Moshi wake hutanabaisha hari ya fumbo na hofu ya Mungu.
Ubani au Uvumba ni ukumbusho wa harufu nzuri ya uwepo wa Bwana wetu Yesu Kristu.
Matumizi ya Ubani huongeza hisia za kuzama katika tafakari wakati wa adhimisho la Misa Takatifu.
Mwonekano wa picha ya Moshi na harufu ya Ubani wakati wa Misa Takatifu inaonyesha Muunganiko wa Mbinguni na duniani.
Hivyo kutufanya kuhisi uwepo wa Mungu.
Moshi humanisha au kuashiria uwepo wa Moto mahali husika na Moto huashiria uwepo wa Mungu.
Utamaduni wa kufukiza Ubani pia hutazamwa kama Sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa na Mungu.
Katika Agano la kale Mnyama aliteketezwa kwa Moto,katika mtizamo kwamba kuchoma kitu ilikuwa ni kumpatia Mungu,pia Moshi wa Ubani ni Ishara ya kupaa kwa Sala na maombi yetu.
Wakati wa adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu,kama Moshi wa Ubani upaavyo Mbinguni ndivyo Sala na maombi yetu hupaa Mbinguni kupitia au kukatiza mawinguni na kumfikia Mwenyezi Mungu katika kiti chake cha Enzi na kuwa harufu nzuri kama Moshi wa Ubani ule.























No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies