YESU KRISTO MTAKATIFU WA MUNGU


TAFAKARI:

YESU KRISTO MTAKATIFU WA MUNGU


Mtume Paulo anaendelea kuwaasa Wathesalonike kutolala usingizi wa imani, kwani wameitwa sio kuzembea kwenye usingizi ila kushirikishwa ukombozi wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyejitoa sadaka kwa ajili ya wamwaminio. Anafundishwa kwamba swala la msingi siku ya ujio wa Kristo, lakini zaidi ni kuendelea kujiandaa siku kwa siku kwa ajili ya kukubalika naye. Wakovu hauji kwa siku ya mwisho tu, kwa matendo ya kila siku yanayoelekea ukombozi. Ndani ya sinagogi Kristo anaonyesha utume huo endelevu anapodhihirisha nguvu yake dhidi ya roho waovu. Kristo anatambulika kama Mtakatifu wa Mungu, na Mkombozi. Yeye mwenyewe anaweka wazi vita dhidi ya roho waovu. Kwa ubatizo tumewekwa huru kutokana na yule muovu. Tunapigani kila siku na roho aliye muovu, lakini kwa msaada ya Kristo Mtakatifu wa Mungu aliye na nguvu ya kushinda maovu, tunashinda maovu.

SALA: Tunapotarajia ujio wako wa pili Ee Bwana, utujalie kukutambua na kukuamini kama Mtakatifu wa Mungu, aliye na nguvu ya kutuweka huru ili kuwa huru kuingia katika ufalme wako.Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies