𝐊𝐖𝐀𝐍𝐈𝐍𝐈 𝐓𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈 𝐑𝐎𝐙𝐀𝐑𝐈

 🌹𝐊𝐖𝐀𝐍𝐈𝐍𝐈 𝐓𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈 𝐑𝐎𝐙𝐀𝐑𝐈???🌹

KWA NINI TUNASALI ROZARY MWEZI WA 5 NA WA 10

Kanisa limeweka mwezi Mei na Oktoba kuwa miezi ya kumweshimu Mama Bikira Maria. Wengi wetu hufahamu tu mwezi Oktoba. Mwezi Mei ni mwezi wa Bikira Maria kwa kuwa Bikira Maria aliwatokea Lucia, Francisco na Jacinta huko Fatima Ureno kwa mara ya kwanza Mei 13, 1917 ujumbe mkuu ukiwa kuhangaikia wokovu wa roho za binadamu kwa njia ya kusali rozari na ibada kwa Moyo Safi wa Bikira Maria.


Mwezi wa 10 ni mwezi wa kusali Rozari Takatifu. Kuchanguliwa kwa mwezi wa 10 kuna msingi wake katika historia ya Kanisa. Waislam wa Kituruki miaka ya 1500 waliamua kutumia mwanya wa vuguvugu la kujitenga kwa Waprotestanti kutoka Kanisa Katoliki. Hivyo waliamua kuvamia nchi za Ulaya ili kueneza dini yao kwa nguvu ya upanga na vita kwa kuwalazimisha Wakristo kuwa Waislam. Oktoba 7, 1571 Waislam wa Kituruki waliamua kuivamia Italy kwa kuanzisha vita ya baharini iliyojulikana kama Vita vya Lepanto (Ugiriki). Baba Mtakatifu wa wakati huo alikuwa Pius V. Baba Mtakatifu alijua wazi kuwa Waislam walikuwa ni wengi kwa idadi kuliko Wakristo na ya kuwa Waislam walikuwa na meli nyingi za kivita kuliko Wakristo. Hata hivyo Baba Mtakatifu aliamuru jeshi lake likisaidiwa na wanajeshi kutoka Spain kwenda baharini kupambana na Waislam. Baba Mtakatifu aliamuru kila askari abebe Rozari na kuisali wanapokuwa vitani majini; pia aliamuru wananchi wa Italia waliobaki majumbani wafanye maandamo makubwa huku wakisali Rozari kuomba msaada wa Bikira Maria ili Wakristo washinde vita. Yeye mwenyewe alisali Rozari siku hiyo ya Oktoba 7. Muda si mrefu habari zilimfikia Baba Mtakatifu kuwa Wakristo wameshinda vita na kati ya meli 242 za Waislam zimesalia meli 12 tu huku jumla ya Waislam 30,000 wakiwa wameuwa, takribani 8,000 wamejeruhiwa au kutekwa. Kwa upande wa Wakristo ni watu 7,500 tu waliokuwa ama wameuawa au wamejeruhiwa au kutekwa ambao baadaye wengi wao walifanikiwa kutoroka. Baba Mtakatifu Pius V alitamka kuwa ushindi huo haujatokana na weledi wa askari wala ubora wa vifaa vya kivita bali ni ushindi uliotokana na maombezi ya Bikira Maria wa Rozari. Kutokana na ushindi huo dhidi ya Waislam Baba Mtakatifu Pius V alianzisha rasmi Sherehe ya Mama Yetu wa Ushindi mwaka 1572. Mwaka 1573 Baba Mtakatifu Gregory XIII aliibadilisha jina sherehe hiyo na kuipa jina la Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu. Mwaka 1884 Baba Mtakatifu Leo XIII alitangaza rasmi kuwa mwezi wote wa kumi utakuwa mwezi wa kusali Rozari Takatifu akiwa na kumbukumbu ya ushindi ambao Wakristo waliupata dhidi ya Waislam katika vita vya Lepanto tarehe 7 Oktoba 1571. Lengo kubwa la kutangaza mwezi wa 10 kuwa mwezi wa Rozari lilikuwa kumweshimu na kumshukuru Mama Bikira Maria ambaye kwa maombezi yake Wakristo walipata ushindi Oktoba 7, 1571


Ikiwa leo ni mwanzo wa mwezi mpya wa Oktoba, mwezi maalumu wa kusali Rozari Takatifu, fahamu sababu za kusali Rozari katika maisha ya Mkristo.

• 𝗦𝗮𝗯𝗮𝗯𝘂 𝗻𝘇𝘂𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗰𝗵𝗲 𝗻𝗶 𝗸𝘄𝗮𝗺𝗯𝗮:-

𝟭. 𝗞𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗮𝗺𝗮𝗻𝗶 𝗱𝘂𝗻𝗶𝗮𝗻𝗶. (𝑩𝒊𝒃𝒊 𝒚𝒆𝒕𝒖 𝒘𝒂 𝑭𝒂𝒕𝒊𝒎𝒂 1917).

𝟮. 𝗞𝘂𝗹𝗶𝗻𝗱𝗮 𝗮𝗺𝗮𝗻𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗳𝗮𝗺𝗶𝗹𝗶𝗮. (𝑷𝒂𝒑𝒂 𝑷𝒊𝒐 𝑿𝑰𝑰)

𝟯. 𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗷𝗮𝘀𝗶𝗿𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗺𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝘀𝗶𝗸𝘂. (𝑷𝒂𝒑𝒂 𝑳𝒆𝒐 𝑿𝑰𝑰𝑰)

𝟰. 𝗡𝗷𝗶𝗮 𝗶𝗹𝗶𝘆𝗼 𝘁𝗮𝘆𝗮𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝘆𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗸𝘂𝗹𝗶𝗻𝗱𝗮 𝗶𝗺𝗮𝗻𝗶. (𝑷𝒂𝒑𝒂 𝑳𝒆𝒐 𝑿𝑰𝑰𝑰)

𝟱. 𝗜𝗻𝗮𝘁𝗶𝗮 𝗺𝗼𝘆𝗼 𝗵𝗮𝘀𝗮 𝘄𝗮𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘄𝗮 𝘀𝗵𝗶𝗱𝗮. (𝑷𝒂𝒅𝒓𝒆 𝑷𝒆𝒚𝒕𝒐𝒏)

𝟲. 𝗞𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝘂𝗹𝗶𝗻𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝘄𝗶𝘀𝗵𝗼. (𝑨𝒔𝒌𝒐𝒇𝒖 𝑯𝒖𝒈𝒉 𝑩𝒐𝒚𝒍𝒆)

𝟳. 𝗜𝗻𝗮𝗽𝗼𝗻𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗼𝘃𝘂 𝘆𝗲𝘁𝘂 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝘀𝗶𝗸𝘂. (𝑷𝒂𝒑𝒂 𝑷𝒊𝒐 𝑿𝑰𝑰)

𝟴. 𝗡𝗶 𝗻𝗷𝗶𝗮 𝗻𝘇𝘂𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗳𝗶𝗸𝗶𝗮 𝘂𝗸𝗮𝗺𝗶𝗹𝗶𝗳𝘂 𝘄𝗮 𝗞𝗿𝗶𝘀𝘁𝗼. (𝑷𝒂𝒑𝒂 𝒀𝒐𝒉𝒂𝒏𝒆 𝑿𝑿𝑰𝑰𝑰)

𝟵. 𝗞𝘄𝗮 𝗮𝗷𝗶𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗳𝗮𝗻𝗶𝗸𝗶𝗼 𝘆𝗮 𝘄𝗶𝘁𝗼 𝘂𝗹𝗶𝗼𝗶𝘁𝗶𝘄𝗮. (𝑴𝒂𝒓𝒔𝒉𝒂𝒍 𝑭𝒐𝒄𝒉, 𝑱𝒆𝒎𝒆𝒅𝒂𝒓𝒊 𝑴𝒌𝒖𝒖 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝑽𝒊𝒕𝒂 𝒚𝒂 𝒌𝒘𝒂𝒏𝒛𝒂 𝒚𝒂 𝒅𝒖𝒏𝒊𝒂)

𝟭𝟬. 𝗡𝗶 𝗻𝗷𝗶𝗮 𝗯𝗼𝗿𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗶𝗽𝗮𝘁𝗶𝗮 𝗡𝗲𝗲𝗺𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗸𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂. (𝑷𝒂𝒑𝒂 𝑷𝒊𝒐 𝑰𝑿)

𝟭𝟮. 𝗞𝘄𝗮 𝗮𝗷𝗶𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗱𝘂𝗺𝘂 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘆𝗮 𝗨𝘁𝗮𝗸𝗮𝘁𝗶𝗳𝘂 𝗺𝗽𝗮𝗸𝗮 𝗺𝘄𝗶𝘀𝗵𝗼. (𝑨𝒔𝒌𝒐𝒇𝒖 𝑯𝒖𝒈𝒉 𝑩𝒐𝒚𝒍𝒆)
𝟭𝟯. 𝗞𝘄𝗮 𝗮𝗷𝗶𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝘂𝘁𝗶𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝗠𝗮𝗺𝗮 𝘄𝗮 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂, 𝗠𝗮𝗹𝗸𝗶𝗮 𝘄𝗮 𝗥𝗼𝘇𝗮𝗿𝗶 𝗧𝗮𝗸𝗮𝘁𝗶𝗳𝘂. (𝑷𝒂𝒑𝒂 𝒀𝒐𝒉𝒂𝒏𝒆 𝑰𝑰)

𝟭𝟰. 𝗡𝗶 𝗸𝗶𝘁𝗶𝘀𝗵𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗺𝗮𝘀𝗵𝗲𝘁𝗮𝗻𝗶. (𝑴𝒕𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊𝒇𝒖 𝑫𝒐𝒎𝒊𝒏𝒊𝒌𝒖𝒔)

𝟭𝟱. 𝗡𝗶 𝘂𝗹𝗶𝗻𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗿𝗼𝗵𝗼 𝘇𝗲𝘁𝘂. (𝑴𝒕𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊𝒇𝒖 𝑫𝒐𝒎𝒊𝒏𝒊𝒌𝒖𝒔)


🌹𝐍𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐊𝐈𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐙𝐈 𝐌𝐖𝐄𝐌𝐀 𝐖𝐀 𝐑𝐎𝐙𝐀𝐑𝐈....🌹

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies