ROZARI TAKATIFU NA LITANIA OCTOBER 1,2023

 JINSI YA KUSALI ROZARI TAKATIFU

Ifuatayo ni mada fupi kuhusu namna ya kusali rozari takatifu ya Bikira Maria, pamoja na sala kuu zinazosaliwa wakati wa sala hii ya rozari.

Wakati wa kusali unaweza kuongeza sala nyingine zifaazo kadri ya nafasi.

Rozari takatifu husaliwa na wakristu kutafakari maisha ya Yesu na Maria yaani Fumbo la Ukombozi, hasa kipindi cha mwezi Mei na Oktoba. Inahimizwa kuisali kama familia kila siku.

Tusali rozari tupate amani, wakosefu waongoke na wasiomjua Yesu Kristu wamjue na kuokoka.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote" au tutolee rozari hii kuwaombea wagonjwa wetu: au :tuwaombee wote walioomba tuwaombee" nk.

Hiyo ni mifano tu. Au unaweza kutoa maombi kuendana na tendo lililotangazwa kwenye kumi husika la tendo la rozari, au namna nyingine itakayofaa.

Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.

Mojawapo ya maneno yafuatayo hutumika:
“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, ……
Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, ……
Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..”

Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,….
Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,….
Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..”

KANUNI YA IMANI
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu.

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, uzima wa milele. Amina.

BABA YETU.
Baba Yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike, utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina

SALAMU MARIA.
Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Na Yesu Mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

ATUKUZWE BABA.
“Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina”

EE YESU WANGU.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi”

TUWASIFU MILELE.
“Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosefu”.

DAMU YA KRISTU.
Damu ya Kristu, iziopoe roho zinazoteseka toharani, izitie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Au;
RAHA YA MILELE.
Raha ya milele uwape ee Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie. Wapumzike kwa amani. Amina.

NB: Kama muda unatosha uimbwe wimbo wa Bikira Maria japo ubeti mmoja kabla ya kutangaza tendo linalofuata (kila baada ya makumi mamoja)

LITANIA YA BIKIRA MARIA


Bwana utuhurumie

Bwana utuhurumie

Kristo utuhurumie

Bwana utuhurumie

Bwana utuhurumie

Kristo utusikie

Kristo utusikilize

Mungu Baba wa Mbinguni,
Utuhurumie

Mungu Mwana Mkombozi wa dunia Utuhurumie

Mungu Roho Mtakatifu
Utuhurumie

Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja Utuhurumie

Maria Mtakatifu~utuombee

Mzazi Mtakatifu wa Mungu~utuombee

Bikira Mtakatifu Mkuu wa mabikira~utuombee

Mama wa Kristo~utuombee

Mama wa neema ya Mungu~utuombee

Mama Mtakatifu sana~utuombee

Mama mwenye usafi wa moyo utuombee

Mama mwenye ubikira
utuombee

Mama usiye na doa utuombee

Mama mpendelevu
utuombee

Mama mstajabivu
utuombee

Mama wa Muumba utuombee

Mama wa Mkombozi
utuombee

Mama wa Kanisa
utuombee

Bikira mwenye utaratibu
utuombee

Bikira mwenye heshima
utuombee

Bikira mwenye sifa
utuombee

Bikira mwenye uwezo
utuombee

Bikra mweye huruma
utuombee

Bikra mwaminifu
utuombee

Kioo cha haki
utuombee

Kikao cha hekima
utuombee

Sababu ya furaha yetu
utuombee

Chombo cha neema
utuombee

Chombo cha kuheshimiwa
utuombee

Chombo bora cha ibada utuombee

Waridi lenye fumbo
utuombee

Mnara wa Daudi
utuombee

Mnara wa pembe
utuombee

Nyumba ya dhahabu
utuombee

Sanduku la Maagano
utuombee

Mlango wa Mbingu
utuombee

Nyota ya asubuhi
utuombee

Afya ya wagonjwa
utuombee

Kimbilio la wakosefu
utuombee

Mtuliza wenye huzuni
utuombee

Msaada wa waKristo
utuombee

Malkia wa Malaika
utuombee

Malkia wa Mababu utuombee

Malkia wa Manabii
utuombee

Malkia wa Mitume utuombee

Malkia wa Mashahidi
utuombee

Malkia wa Waungama dini utuombee

Malkia wa Mabikira
utuombee

Malkia wa Watakatifu wote utuombee

Malkia uliyepalizwa Mbinguni utuombee

Malkia wa Rozari takatifu utuombee

Malkia wa amani
utuombee

Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,
Utusamehe ee Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,
Utusikilize ee Bwana

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,
Utuhurumie.

Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe:
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.

SALAMU MALKIA.
Salamu Malkia, Mama mwenye huruma, uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu. Tunakusihi hapa ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi, Mwombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, ee mwema, ee mpendelevu, Bikira Maria.

KUMBUKA.
Kumbuka, ee Bikira Maria mwenye rehema, tokea zamani zote haitambulikani kumeachwa mwenye aliyekimbilia ulinzi wako, mwenye aliyetaka msaada wako, mwenye aliyetaka maombezi yako. Nami nimetumaini kwako, nimekimbilia kwako, ee Mama yangu, Bikira asiye na mfano, nimekuja kwako, nasimama mbele yako mimi mwenye dhambi. Mama wa Neno wa Mungu, usiyachukie maneno yangu, uyapokelee, uyasikilize, ukanifanyizie. Amina.

SALA KWA MTAKATIFU YOSEFU.

Ee Mt. Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira Mtakatifu Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza Mtoto Yesu, twakuomba sana, utuangalie kwa wema sie tuliokuwa fungu lake Yesu Kristu, tukakombolewa kwa damu yake.
Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako.
Ee Mlinzi amini wa jamaa takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristu. Ee Baba uliyetupenda mno tuepushe na kilema chochote cha madanganyo na upotevu.

Ee kinga yetu mwezaji, utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwopoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi likinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote; mtunze daima kila mmoja wetu, tufwate mfano wako, ili tupate na msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni makao ya raha milele. Amina.

TUNAUKIMBILIA.
Tunaukimbilia, ulinzi wako, Mzazi Mtakatifu wa Mungu. Usitunyime tukikuomba katika shida zetu, utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, ee Bikira mtukufu na mwenye baraka. Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies