NOVENA KWA MT;MIKAELI MALAIKA MKUU




NOVENA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU NA MAKUNDI TISA YA MALAIKA. 

Novena hii pia husaliwa tarehe 20/9 hadi tarehe 29/9 sikukuu ya malaika wakuu. NB:Kwa kila siku ya novena hii Sali sala ya mwanzo kutoka katika novena kwa mtakatifu Raphaeli kisha taja neema unayoomba kwa maombezi ya malaika mkuu Mt Mikaeli na makundi tisa ya malaika kumbuka pia kusali Rozari ya Mt. Mikaeli ukimaliza sali sala zifuatazo kutokana na siku husika : 

Siku ya kwanza: kwa heshima ya kundi la Seraphimu Mtukufu mkuu sana wa jeshi la mbinguni Mt. Mikaeli malaika mkuu utulinde katika vita dhidi ya wakuu na wenye nguvu dhidi ya nguvu za juu za ulimwengu huu wa giza dhidi ya Roho za kishetani zizungukazo angani,uelekeze msaada wako kwa watu ili Mungu awekwe katika sifa zake na uziondoe kutoka katika mikono ya mashetani wasio haki. AMINA

 Siku ya pili: kwa heshima ya kundi la Kerubim Mtakatifu Mikaeli mkuu wa majeshi ya malaika ninakuita ili unisikie ninakuomba uchukue Roho yangu siku ya mwisho chini ya ulinzi wako mtakatifu na uichukue katika mapumziko ya amani na utulivu ambapo Roho za watakatifu zinasubiri siku ya furaha ya mwisho siku ya hukumu utukufu na ufufuko ili nitakapo ongea au kubaki kimya nitakapoamka au nitakapo tembea au nitakapo simama kwa mapumziko unilinde nimalize kazi zangu zote katika maisha yangu uniokoe kutoka katika majaribu ya shetani na moto wa milele. AMINA 20

 Siku ya tatu: kwa heshima ya kundi la wenye enzi Mlinzi mkubwa wa wakiristu Mt. Mikaeli malaika mkuu kwa kujazwa na utulivu na kwa kazi uliyopewa ya kulilinda kanisa kusawazisha mabishano dhidi ya dini na utengano katika kanisa uwatenganishe wasioamini zidisha ushindi dhidi ya watenda mabaya wanaotaka kuharibu imani yetu ili kwamba kanisa la Yesu Kristu likaribishe waumini wapya na imani mpya kwa kanisa zima ili tuweze kushiriki mbinguni na Roho zilizochaguliwa katika utukufu mkubwa wa Mkombozi wa kimungu, ambapo kwake unapata ushindi wako na mafanikio yako. AMINA

 Siku ya nne: kwa heshima ya kundi la watawala. Mtakatifu Mikaeli wewe ambae ni mkuu na mchukuaji asiyebadilika wa malaika wazuri nisaidie kila mara katika upole wako dhidi ya jeshi la malaika wagiza niokoe ili kupitia ulinzi wako nishiriki mwanga wa malaika wema mbele ya kiti cha thamani cha hukumu, uwe mlinzi wangu nikubalie mwili wangu na unisaidie dhidi ya hasira ya haki ya watenda mabaya ili kupitia katika kazi zangu katika mapumziko yangu mchana na usiku nipatie mafanikio na ili mawazo yangu yawe tayari kwa ajili ya kazi za Mungu. AMINA

 Siku ya tano: kwa heshima ya kundi la wenye nguvu Mt.Mikaeli Malaika mkuu wewe ambaye ni mwongozaji na mlinzi wa kanisa kwako mungu alianzisha kazi ya kupeleka mbinguni roho mpya ili zimeheshimu utuombee ili Mungu wa amani aweze kumharibu shetani katika miguu yetu ili kwamba asiweze kuwa tayari tena kuwafunga watu katika minyororo na kuharibu kanisa chukua sala zetu mbele ya Mungu ili kwamba bila mwisho Bwana atujalie sisi huruma yake wewe ulimwangusha nyoka ambaye ni shetani na muovu na kumtupa motoni ili asiweze tena kuyaangusha mataifa. AMINA

 Siku ya sita: kwa heshima ya kundi la wenye mamlaka Mt Mikaeli Malaika mkuu utulinde katika vita ili kwamba tusiweze kuwekwa katika mateso siku ya hukumu ya kweli mtukufu mkuu sana utukumbuke sisi kila sehemu na kila mara ulipopigana na nyoka tulisikia sauti za watu kutoka mbinguni zikisema ukombozi heshima na utukufu 21 kwa mungu mwenye nguvu bahari ikanyanyuka dunia ikatikisika uliposhuka kutoka mbinguni kuja kusaidia watu wa Mungu. Amina. 

Siku ya Saba: kwa heshima ya kundi la wakuu Mt. Mikaeli Malaika Mkuu mara tatu ya watakatifu wa jeshi takatifu uliyewezeshwa na Mungu kupanga na kuongeza makundi tisa ya malaika yenye heshima nzuri kuliko makundi yote ya dini yenye sifa zote nakuomba uwashe fikra zangu za ndani safisha moyo wangu Maskini ulioshambuliwa na mabonde ya maisha uniamshe roho yangu iliyo katika mambo ya ulimwengu mpaka katika hekima ya mbinguni.usiniruhusu kuacha kufuata maelekezo yanayonielekeza kwenda mbinguni ponya madonda ya roho yangu ondoa mateso yangu yote na kutopatia faida na mikosi yangu yote. AMINA. 

Siku ya nane: kwa heshima ya kundi la malaika wakuu Malaika mkuu mtakatifu Michael wewe uliyepewa kazi ya kupokea maombi yetu na kutoongoza katika vita vyetu na kubeba roho zetu ninailipia nyumba ya moyo wako ambayo ni kama ya Mungu baada ya neno lake la kimungu kwamba hamna Roho nyingine ya mbinguni itakayokuwa sawa na yako. Kwako nguvu zisizoesabika kwa wale watu wote wenye ibada kwako wanaungana na mioyo ya mama maria mkingiwa dhambi ya asili na wa yesu kristu kwa uzuri wa kibinadam nilinde dhidi ya maadui wa Roho yangu na mwili wangu nifanye niweze kuhisi furaha na uhuru wa msaada wako usioonekana na matokeo ya ulinzi na sala zako AMINA.

 Siku ya tisa: kwa heshima ya kundi la malaika Mtukufu malaika mkuu wa Mikaeli mwangushaji wa shetani kwa niaba ya Mungu na mlinzi wa kanisa katoliki wewe ambaye nguvu zote za kazi ya kupokea roho pindi zinapoachana na mwili na kuzitpeleka katika hukumu, ni zako unisaidie katika vita yangu ya mwisho pamoja na malaika mlinzi wangu mzuri njoo katika msaada wako kutupilia mbali roho zote mbaya usiruhusu roho hizo zinijaribu unifunze katika imani yangu na matumaini yangu na mapendo ili kwamba roho yangu ichukuliwe nawe katika hukumu baada ya hukumu unipeleke katika 22 sehemu yangu ya mapumziko ili kushiriki umungu pamoja na mwokozi pamoja na roho zilizobalikiwa. AMINA.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies