SALA YA NOVENA KWA AJILI YA ROHO ZA MAREHEMU

SALA YA NOVENA KWA AJILI YA ROHO ZA MAREHEMU WALIOKO TOHARANI.

 Baba Mungu mwenye huruma nikiungana na marehemu washindi wa kanisa walioko mbinguni, ninakuomba uzionee huruma roho zote zilizomo toharani.nakuomba uzifikilie katika matendo yako ya upendo na zioneshe huruma roho hizo kwa ajili ya mapendo wa mwanao Yesu Kristu yasiyokuwa na mwisho tafadhali sana ninakuomba uziweke huru roho hizo kutoka katika maumivu na mateso na uziweke roho hizo ziweze kufurahia amani na furaha ya milele. Mungu Baba wa mbinguni ninakushukuru kwa neema ya kuwatunza ambayo unawapatia wale wote walioanguka katika imani. Mwokozi mpendwa Yesu Kristu, wewe ni mfalme wa wafalme katika ardhi ya mbinguni. 

Ninakuomba wewe kwa kupitia huruma yako uweze kusikiliza sala yangu na kuziweka huru roho zote zilizomo toharani hasa roho zote za watu waliokufa, wanaokufa, watakaokufa, wanaoendelea kufa na pia tunaomba uzipokee roho zetu tutakapokufa, utuongoze kutoka katika geneza la giza na kuzipeleka roho hizo katika nuru na uhuru wa watoto wa Mungu katika ufalme wa utukufu wako. Mwokozi mpendwa, nakushukru kwa kwa kuziokoa roho za maskini kwa damu yako ya thamani na kuzisaidia kutoka katika adhabu ya kifo.

 Mungu roho mtakatifu, uwashe kwangu moto wa mapendo yako ya kimungu. Nakuomba ukuze imani na ujasiri wangu na kwa utukufu  wako, kubali sala zangu ninazo kutolea kwa ajili ya roho zilizomo Toharani. Ninatumaini kupata na kusambaza ibada hii kwa kanisa zima lakini hasa kwa roho za marehemu wazazi wetu, kaka zetu, dada zetu ndugu na marafiki zetu wote waliokufa. Sikiliza sala yangu ili niweze kuungana nao katika utukufu wa ufalme wako. Mungu Roho Mtakatifu, ninakushukru kwa neema zote na roho zote ulizotakatifuza ulizozipa nguvu na kuziokoa na hasa kwa kuzifariji katika mateso yao walionayo sasa. Naomba baadaye waungane na wewe na kusikia maneno yaliyobarikiwa ambayo yatawaita katika nyumba ya mbinguni “njooni nyinyi mliobarikiwa na Baba yangu mrithi, ufalme ulioandaliwa kwenu”. AMINA.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies