SALA ZA MUHIMU


SALA TATU NZURI SANA.

 Sala hizi zinafaa sana kwa mtu anayekufa kama kuomba HURUMA. Sali BABA YETU, kisha sali sala zifuatazo:- 

1. SALA: Bwana Yesu Kristu, Mwana wa Mungu na wa Bikra Maria, Mungu na mtu, uliyetoka jasho la damu kwenye mlima wa mizeituni ili kuleta amani na kumtolea Mungu Baba wa mbinguni kwa wokovu wa watu hawa waliokufa, wanaokufa, watakaokufa na wale wote wanaoendelea kufa. Sisi wenyewe utujalie kufa kifo chema. Tunawaombea wagonjwa waliopo mahospitalini na majumbani afya njema ya mwili na roho, wafungwa gerezani, tunauwaombea ulimwenguni mzima na dini zote, tuziombea familia zetu zote, tunawaombea wale wote wanaohasi dini zao na kwenda katika dini nyingine, tunawaombea wazazi wote wawalee watoto wao katika maadili yanayostahili mbele ya Mwenyezi Mungu na tunawaombea watoto wote uwajalie neema ya kuwapenda, kuwaheshimu, kuwatii, na kuwasaidia wazazi wao ili kile ulichowaahidia yaani miaka mingi hapa duniani na heri mbinguni wakipate. Tunamuombea Rais wetu 37 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ………….aweze kuongoza nchi yetu kwa amani. Pia tumuombee mtumishi muweza kumsaidia na kumfariji katika magumu yote anayokutana nayo katika kazi zake za kuokoa roho na tunakuomba utuondolee hukumu kama kwa ajili ya dhambi zetu tuliyostahili. Ee Baba wa milele, tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu, mwanao anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu sasa na milele. AMINA.

 2. SALA Bwana Yesu Kristu wewe uliye kufa kwenye mti wa msalaba kwa ajili yetu ukimtolea mapenzi yako Baba yako wa mbinguni ili kuleta amani na kumtolea kifo chako kitakatifu sana Baba wa mbinguni ili kuwafungulia watu hawa waliokufa, wanaokufa watakaokufa na wale wote wanaoendelea kufa. Na sisi wenyewe utujalie kufa kifo chema na kutuficha kutoka kwenye adhabu tulizostahili kwa dhambi zetu, utujalie hili ee Baba wa milele, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu mwanao anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu, sasa na milele. AMINA.

 3. SALA: Bwana Yesu Kristu wewe uliyenyamaza kimya ukaongea kwa vinywa vya manabii, nimekuvutia kwangu kwa njia ya upendo milele, upendo uliokuvuta toka mbinguni hata mwili mwa Bikra, upendo uliokuvuta toka mwilini mwa Bikra hadi duniani upendo uliokufanya uishi miaka 33 duniani kama alama ya upendo mkuu umetupatia mwili wako kama chakula cha kweli na damu yako kama kinywa cha kweli kama alama ya upendo mkuu umekubali kuhukumiwa kifo kufa, kuzikwa na ukafufuka kweli ukamtokea mama yako mtakatifu na mitume mtakatifu na kama alama ya upendo mkuu umepaa kwa nguvu na uwezo wako na kukaa mkono wa kuume wa Baba Mungu wa mbinguni nawe umemtuma roho wako mtakatifu mioyoni mwa mitume mwako na moyoni mwa wote wanaokutumainia na kukuamini kwa njia ya alama yako ya upendo wa milele basi funga mbingu leo na kuwachukua watu hawa waliokufa, wanaokufa watakaokufa na wale wote wanaoendelea kufa na sisi wenyewe utujalie kufa kifo chema na kutuondolea dhambi zetu zote ili tuweze kufurahi pamoja nawe milele na milele. AMINA.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies