MASOMO YA MISA, DESEMBA 10, 2023

DOMINIKA YA 2 YA MAJILIO MWAKA B



MWANZO:
Isa. 30:19, 30
Enyi watu wa Sayuni, Tazameni Bwana atakuja kuwaokoa mataifa; naye Bwana atawasikilizisha sauti yake ya utukufu katika furaha ya mioyo yenu.


SOMO 1
Isa. 40:1-5, 9-11

Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umechiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dahmbi zake zote.

Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu, Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.

Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, panda juu yam lima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.

Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, tahawabu yake I pamoja naye, na ijara yake I mbele zake. 

Atalilisha kundi lake kama mchungaji, atawakusanya wanakondoo mikononi mwake; na kuwachukua kifuani mwake, nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI
Zab. 85:8-13 (K) 7

(K) Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, utupe wokovu wako.

Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, 
Maana atawaambia watu wake amani,
Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu. (K)

Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na amni zimebusiana.
Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni. (K)

Naam, Bwana atatoa kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki itakwenda mbele zake,
Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia. (K)


SOMO 2
2Pet. 3:8-14

Wepenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia,  bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo makuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. Kwa hiyo, wapenzi kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidi ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


SHANGILIO
Lk. 3:4, 6

Aleluya, aleluya,
Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake. Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.
Aleluya.


INJILI
Mk. 1:1-8

Mwanzi wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake.
Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu. Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtatifu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies