MOYO ULIYO SAFI!


Tukiangalia katika somo la Injili ya leo tunaweza kushangazwa na maneno makali ya Yesu. “ngoa jicho lako” au “ukate mkono wako na kuutupa mbali”. Yesu alitumia lugha hii kali ili aweze kuweka mbele ya wafuasi lengho moja katika maisha ambalo ni maisha safi ya sadaka- hii ikiwa ni muunganiko wa matakwa yetu na Mungu. Kama Daktari anavyoweza kuondoa mguu au sehemu ya mwili kwamanufaa ya mwili mzima, nasi pia tunapaswa tuwe tayari kuachana na kile kinachoweza kutufanya tutende dhambi, na ambacho kwa njia yeyote kitatuletea kifo cha roho zetu. Yesu pia anatuonya sisi pia tuwe na jukumu kubwa la kutokuwa kikwazo au kisababishi cha kuwafanya wengine watende dhambi, au kuwaangusha, tusiwe kipingamizi au tusitoe mfano mbaya ambao utawaongoza wengine kwenye dhambi. 


Pili, Yesu anatufundisha kwamba kuwa safi ni pamoja nakuwa tayari kukabili kila hali katika maisha katika hali ambayo inatimiza sheria ya Mungu, si tu katika matendo ya njee bali naya ndani pia. Yesu anasema tamaa mbaya hutoka moyoni. Ndio maana dhambi yakukosa uaminifu ni lazima itibiwe kwanza kutoka ndani ya moyo, sehemu ambayo si ya hisia tuu, bali utashi, maamuzi, mawazo, na malengo pia. Ni lazima tutambue lengho la Amri za Mungu na tuamue kutoka moyoni kumfuata Mungu. 

Sala: Baba wa Mbinguni, nitakase mimi, ili niweze kufanana na Kristo mwanao kwa maisha yangu. Amina.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies