MPENDE ADUI YAKO!

 



MPENDE ADUI YAKO!

Katika Injili ya Leo Yesu anatupa changamoto kwa kutupa kazi ngumu, anawaambia wafuasi wake “wapendeni adui zenu na waombeeni wanao wadhulumu”. Kwa njia hii anatualika sisi tuwe kama yeye, kuwa sura yake kwakuwaombea wote, kuwapenda wote kama yeye alivyofanya. “kwani Mungu huwapa watu wote jua lake, wazuri na wabaya, mvua ya Mungu huwanyeshea walio na haki na wasio na haki”.

Injili inataka kutuonesha sisi kwamba, Mungu anafunuliwa kila wakati na kwakupitia watu wengi. Ni jukumu letu binafsi na kama jumuiya kuwa tayari, kuwa wazi ili kumuona Mungu tunapokutana na hali mbali mbali za Kimungu katika maisha yetu. Mungu wetu ni Mungu wa nafsi. Kila mara sura yake hubadilika ndani yetu na kutufanya sisi tuwe watimilifu.

Tutafakari juu ya wale wote ambao tunapata wakati mgumu kuwapenda. Anaweza kuwa ndugu wa familia, mmoja wa wafanyakazi wenzako, jirani yako au mmoja ya mtu ambaye mlikosana zamani na humjapatana. Ukishamtambua huyo mtu, jiulize kama unamuombea, ulisha Sali kumuombea? Je ulisha tumia muda Fulani kusali na kumwombea? Unasali ili Mungu awamiminie huruma yake na neema yake? Inaweza kuwa vigumu kuonesha upendo na huruma kwao, lakini sio vigumu kusali kwa ajili yao. Kusali kwa ajili ya walio tuumiza ni ufunguo wa kumruhusu Mungu alete mapendo ya kweli na hali ya kuwajali katika mioyo yetu. Ni sehemu ya kumruhusu Mungu abadili hisia zetu juu yao ili tusiwe tena na chuki juu yao na kuwachukia. Jiweke katika hali ya kusali na kumuombea mtu ambae unamchukia sana. Sala hii haina maana itabadili jambo hili kwa usiku mmoja, lakini kama utajikita katika sala ya namna hii kila siku, taratibu Mungu atabadilisha hali yako ya Moyo na kukuondolea mzigo wa hasira na maumivu ulio umizwa ambayo yanaweza kukuweka mbali na upendo wake ambao anataka uwe nao kwa watu wake.

Sala: Bwana, nina Sali kwa ajili ya mtu ambaye unapenda mimi nimwombee. Nisaidie niweze kuwapenda watu wote na zaidi sana kuwapenda wale ambao naona vigumu kuwapenda. Badilisha hisia na mtazamo wangu juu yao na nisaidie niweze kuwa huru kutoka katika kila aina ya hasira. Bwana, naomba unisaidie nikutane na wewe ili niweze kuwa kama wewe. Yesu, nakuamini wewe. Amina

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies