MTAKATIFU WA LEO 17 JULY
Leo Julai 17, Kanisa linamkumbuka Mtakatifu Pambo Mkaa Pweke (390)
Inasemekana kuwa Pambo alizaliwa huko Misri, na katika ujana wake aliwahi kuwa mfuasi wa Mt.Antoni mkaa pweke jangwani uko Misri (tazam 17 Januari). Alisisitiza kufanya kazi za mikono, kwa desturi alisuka mikeka kutokana na majani ya michikichi. Alifunga na kusali kwa muda mrefu . Zoezi kubwa hasa alilofanyakatika maisha yake ni kuutawala ulimi wake kwa kukaa kimya na kufikiri kwanza kabla ya kusema. Wakati mwalimu wake alipompa somo kutoka zaburi 39 “Nalisema nitazitunza njia zangu nisije nikakosa kwa ulimi wangu”, Pambo alijibu: “Hii itatosha kwa leo”. Akaenda jangwani kufikiri juu ya maneno hayo. Alipomaliza kutafakali juu ya maneno hayo kwa miezi sita, alirudi tena kuendelea na ,masomo yake.
Mt. Melania mjane aliye fungua nyumba ya Kitawa huko Yerusalemu, alimtembelea Mt. Pambo, na kumletea zawadi ya pauni Mia Tatu za sarafu. Alipozipokea , alisema kuwa zingeweza kutumika kwa ajili ya monasteri maskini, lakini hakushukuru. Melania alimkumbusha kwa upole :”Kuna pauni mia tatu za salafu, baba yangu”.MT. Pambo alijibu :”Yule aliyemtolea zawadi hii, hana lazima yako wewe umwambie ina thamani gani”. Na wakati mwingine alipoombwa ahesabu fedha aliyopewa ili akaigawe, alisema “Mungu haulizi ni kiasi gani, bali zimetolewaje na kwania gani”.
Pambo alifariki akiwa anasuka kikapu. Alisema:”Tangu nilipokuja jangwani , sijala chochote ambacho sijakifanyia kazi,na sikumbuki kama hata mara moja nilisema kitu chochote ambacho nilikisikitikia baadaye”. Mt. Melania alikuwepo alipokufa; alikuwepo pia kwenye mazishi yake, na akachukua kikapu kilichukua kikapu kilichokuwa kinashonwa na Mt. Pambo kama mabaki ya thamani kubwa.
No comments
Post a Comment