JUMAPILI DOMINIKA 28 MTAKATIFU EDWARD, MUUNGAMA DINI

 MTAKATIFU EDWARD, MUUNGAMA DINI

13 OKTABA
Mtakatifu Edward alizaliwa mwaka 1005 huko Islip, Oxfordshire - Uingereza. Alikuwa mtoto wa Mfalme Ethelred na Mke wake Emma. Alikimbia uvamizi uliofanywa na Canute mwaka 1013.Akaenda Ufaransa. Mfalme Ethelred alikufa mwaka 1016.Canute akamuoa Emma, na akawa mfalme wa Uingereza.
Mwaka 1042 Edward alirejea Uingereza ,na kwa msaada wa Earl Godwin akatangazwa mfalme wa Uingereza. Mwaka 1044 Edward alimuoa binti wa Godwin.
Katika maisha yake Mtakatifu Edward ,aliendesha utawala bora na wa haki.Akamaliza migogoro ambayo ingeleta vita kwa majadiliano.
Mtakatifu Edward aliamua kuacha madaraka na kumpa mtu mwingine.Yeye aliamua kumtumikia Mungu.
Akajenga nyumba ya watawa katika mji wa Westminster. Akasaidia kueneza neno la Mungu, mpaka alipokufa tarehe 5 Januari 1066, huko London, Uingereza.
Mtakatifu Edward alitangazwa Mtakatifu mwaka 1161 na Papa Alexander III.
Watakatifu na Wenyeheri wanaokumbukwa leo ni :
M/h. Alexandrina Maria da Costa
Mt. Berthoald
Mt. Carpus
Mt. Chelidonia
Mt. Colman wa Stockerau
Mt. Comgan
Mt. Faustus
Mt. Fyncana
Mt . Gerald wa Aurillac
Mt. Maurice wa Carnoet
Mt. Regimbald
Mt. Romulus
Mt. Theophilus wa Antioch
Mt. Venantius
Mtakatifu Edward, Watakatifu na Wenyeheri wote mtuombee kwa MUNGU ili tusimame imara katika Imani Katoliki.
No photo description available.
All reactions:

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies