MASOMO YA MISA JUMATATU 14 OKT 2024

JUMATATU JUMA 28 LA MWAKA 

SOMO I

Gal.4:22-24,26-27,31-5:1

Imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili. Mmoja alikuwa mjakazi na mwingine alikuwa muungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa muungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, mmoja kutoka Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni hajiri. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, furahi wewe uliye tasa, usiye zaa; paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu: maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi kuliko huyo aliye na mume. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana. Katika ungwana huo Kristo alituandikia huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.


WIMBO WA KATIKATI: Zab.113:1-7(K)2

Aleluya

1. Enyi watumishi wa Bwana sifuni

Lisifuni jina la Bwana

Jina la Bwana lihimidiwe

Tangu leo na hata milele.


(K) Jina la bwana lihimidiwe milele.


2. Toka mawio ya jua hata machweo yake

Jina la bwana husifiwa

Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote

Na utukufu wake ni juu ya mbingu. (K)


3. Ni nani aliye mfano wa bwana

Mungu wetu aketiye juu

Anyenyekeaye kutazama

Mbinguni na duniani?

Humwinua mnyonge kutoka mavumbini

Na kumpandisha masikini toka jaani. (K)


SHANGILIO: Zab.119:34

Aleluya, aleluya!

Unifahamishe nami nitaishika sheria yako. Nitaitii kwa moyo wangu wote,

Aleluya!

INJILI: 

Lk.11:29-32

Makutano walipokuwa wakimkusanyikia, Yesu alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki. Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka nchi za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.

Neno la Bwana..............




No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies