LEO NOVEMBA 13 KUMBUKUMBU YA MT.STANISLAUS KOSTIKA

NOVEMBA 13  KUMBUKUMBU YA MT.STANISLAUS KOSTIKA 

MAISHA YA WATAKATIFU 


Mtakatifu Stanislaus, alizaliwa mwaka 1550 mwezi Oktoba 28, huko Rostkowo, Poland. Alikuwa mtoto wa 2 kati ya watoto 7 wa familia hiyo yenye kuheshimika. Akiwa na miaka 14 yeye na kaka yake walijiunga na chuo cha Wa Jesuit huko Vienna.
Akiwa Vienna, alipata matatizo ya afya na hivyo kuugua mara kwa mara.Aliishi maisha safi na alipata maono mbalimbali.Katika maono hayo, Mama Maria, alimwambia ajiunge na shirika la Wa Jesuit. Alishauriwa na Mtakatifu Peter Canisius, ambaye alikuwa mkuu wa Wa Jesuit huko Ujerumani, kuomba kujiunga na shirika hilo huko Roma, Italia. Mtakatifu Stanislaus, aliamua kwenda Roma, japo ilikuwa safari ndefu na ya kuchosha.Pia njiani kulikuwa na hatari nyingi mno. Hata hivyo, alifika Roma tarehe 25 Oktoba 1567.Hapo alijiunga na shirika.
Katika muda mfupi alipokuwa hapo, alionyesha utofauti mkubwa sana , akitumia muda wake mwingi kwa sala ,kufunga na majitoleo mbalimbali. Lakini afya yake haikuwa njema na alipata homa kali siku ya tarehe 15 Augusti mwaka 1568, Inasemekana alitabiri kifo chake siku chache kabla hakijatokea.Mtakatifu Stanislaus alikufa akiwa anasali, alfajiri saa 10.
Alitangazwa Mwenyeheri mwaka 1605 na akatangazwa Mtakatifu mwaka 1726 tarehe 31 Desemba huko Roma, Italia.

No comments

Post a Comment

Shajara Yetu © all rights reserved
MKATOIKI KIGANJANI by mitume technologies